Nape aipa tano kurugenzi mawasiliano Ikulu, habari maelezo

Nape aipa tano kurugenzi mawasiliano Ikulu, habari maelezo
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amezipongeza Kurugenzi za Mawasiliano Ikulu na Idara ya Habari Maelezo kwa ubunifu wanaouonesha katika kuelezezea mafanikio ya Serikali kwa kutumia teknolojia mbalimbali za habari na mawasiliano.
Nape ametoa kauli hiyo siku moja baada ya kumwagiza mkurugenzi wa habari maelezo, kufuatilia utendaji kazi wa maofisa habari na mawasiliano wote ili kuona kama utendaji wao unaleta tija kwa jamii.
Akizungumza leo (Jumatano) Waziri Nape amesema licha ya changamoto ya vifaa vinavyowakabili maafisa mawasiliano wa Serikali, kurugenzi za mawaziliano Ikulu na idara ya habari maelezo wamekuwa wanafanya kazi nzuri za kuisaidia Sarikali.
“Nawapongeza wakurugenzi vijana, Dk Hassan Abbasi (Maelezo) na Grayson Msigwa wa Ikulu. Hawa ni mfano wa ubunifu wa namna Serikali inavyoweza kutumia teknolojia mbalimbali za mawasiliano katika kuhakikisha mazuri yanayofanywa na Serikali yanatangazwa, yanaenezwa na kutetewa,”amesema Nape.


DOWNLOAD APPS YA TZTOWN HAPA

http://ift.tt/2ms2574
WANANCHI WAOMBA SERIKALI KUODOA TAKA KIZIMBANI MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE


from Blogger http://ift.tt/2m3IDlY
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2nHGCrI
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2m46yS5
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2mw1YHv
via IFTTT