KATIBU WA CHAMA CHA WALIMU MKOA WA NJOMBE FRATERN KWAHHISON AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE LEO
WANAFUNZI WAPO KWENYE MCHEZO WANAOELEKEZWA NA MWALIMU WAO BAADA YA KUTOKA DARASANI
MWALIMU MWALONGO WA SHULE YA MSINGI MPECHI AKIZUNGUMZA KUHUSIANA NA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI
MWALIMU AKIWACHEZESHA WANAFUNZI KWA KUNYOSHA VIUNGO BAADA YA KUTOKA DARASANI
Serikali Mkoani Njombe inakabiliwa na deni la zaidi ya shilini milioni za malimbikizo mbalimbali ya mishahara ya walimu ya mwaka 2015 na 2016 ikiwemo fedha za uhamisho pindi wanapohamishiwa sehemu nyingine.
Kauli hiyo imetolewa na katibu wa chama cha walimu mkoa wa Njombe Mwalimu Fratern Kwahhison wakati akizungumza na Uplands fm kuhusiana na siku ya mwalimu Duniani ambayo Kitaifa Chama hicho huadhimisha baada ya miaka mine.
Mwalimu Kwahhison amesema sherehe hiyo inatoa fursa kwa walimu kuwasilisha madai na changamoto mbalimbali kwa serikali ili kuishinikiza iweze kuwatatulia kwa wakati na walimu hao wafanye kazi katika mazingira yasiyo na manung’uniko yoyote.
Amesema walimu wa Tanzania wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kulipwa mshahara mdogo usiyokidhi mahitaji yao,kutopandishwa madaraja na kurekebishiwa mishahara,kutolipwa madeni yao na kushindwa kuwajengea nyumba za kuishi ambapo walimu wengi wanatoka umbali mrefu wa kilomita zaidi ya tano.
Mwalimu Kwahhison amebainisha viwango tofauti vinavyodaiwa na walimu kwenye halmashauri za Mkoa wa Njombe kuwa serikali inadaiwa na walimu wa mji wa Makambako milioni 30580900,Wilaya ya Njombe inadaiwa milioni 38386800, Wilaya ya makete inadaiwa shilingi milioni 223946516,Halmashauri ya wilaya ya ludewa inadaiwa shilingi milioni 419089346,Wanging’ombe milioni 188603507,na Halmashauri ya Mji wa Njombe inadaiwa shilingi milioni 254645090 madai hayo yote ni sehemu tu kwani bado wanaendelea kukusanya madai hayo.
Mwalimu huyo Kwahhison amesema madai hayo ni yale ya Likizo,ya matibabu,upandishwaji madaraja,uhamisho,kuwasafirisha walimu wastaafu baada ya kumaliza kipindi chao cha utumishi serikalini,madai ya shughuli maalumu pindi wanapoitwa na mwajili wao, kujikimu,ajira mpya,mazishi na mapunjo.
Kwa upande wao baadhi ya walimu mjini Njombe wametaka serikali kuwaboreshea mazingira ya kufanyia kazi ikiwemo vitendea kazi ,kuongeza idadi ya walimu kwa baadhi ya shule zenye walimu wachache pamoja na kuwajengea nyumba za kuishi ili kufundisha vizuri wanafunzi.
Mashirika ya UNESCO na ILO Yalianzisha siku ya mwalimu Duniani mwaka 1994 lengo likiwa ni siku ya kumbukumbu na kutafakari madhila wanazopata walimu katika utumisho wao kutokana na waajili wakorofi ambao hawataki kuwapa haki.
Maadhimisho hayo kwa mwaka huu hapa nchini yamefanyika kwa baadhi ya mikoa ukiwemo mkoa wa Luvuma yakiwa na Kauli mbiu inayosema Mwalimu athaminiwe