MWANAFUNZI APIGWA NA WAALIMU SITA MPAKA KULAZWA



SIKU chache baada ya kutokea tukio la kushambuliwa mwanafunzi ikiwa kama adhabu mkoani Mbeya katika shule ya Sekondari Kutwa ya Mbeya, waalimu sita wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Njombe baada ya kudaiwa kumshambulia mwanafunzi wa kike wa kidato cha nne kwa kosa la kukutwa na simu ya mkononi katika begi lake la chuma (Tranka) la nguo na waalimu wake.

Mwanafunzi huyo wa shule ya binafsi ya sekondari ya Mbogamo, ya mkoani Njombe, Elizabeth Simfukwe inadaiwa kushambuliwa na mkuu wa shule akiwa na waalimu wengine na kumsababishia maumivu kisha kulazwa katika Hospitali ya Kibena mkoani Njombe kwa siku zaidi ya tatu akipatiwa matibabu.
Elimtaa Media imefika katika Hospitali ya Kibena inazuiliwa kumuona mwanafunzi huyo na kuwa bado anapatiwa matibabu na anaendelea vizruri huku akiwa amelazwa hapo kwa zaidi ya siku tatu tangu Oktoba 6 mwaka huu alipo patiwa kipigo hicho.

Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Selina Nyoni, anasema kuwa kweli mtoto huyo amelazwa katika Hospitali hiyo lakini kuna maelezo kutoka juu hairuhusiwi kuonana na mtu yoyote kwa kuwa mtoto hiyo hajafa.

“Mtoto huyu amelaza hapa siku ya tatu anaendelea vizuri lakini kuna maelezo nimepata hairuhusiwi mtu yeyote kumona na hairuhusiwi habari zake kutolewa kwa kuwa jamo hili lina gusa jamii na huyu ni mtoto,” alisema Dr Nyoni.

Kwa mujibu wa Dr Nyoni anasema kuwa mwanafunzi huyo aliletwa hapo baada ya kupigwa na waalimu wake kwa viboko baada ya kukutwa na simu ya mkononi ambapo inadaiwa kuwa alikuwa hataki kueleza anawasiliana na nani kupitia simu hiyo ndipo waalimu wakaanza kumuazibu kwa viboko.

Mwanafunzi Elizabeth (19) wa kidato cha nne chanzo cha kupigw ana waalimu 6 kwa kuchangiana inadaiwa ulipita ukaguzi shuuleni hapo na kupatikana na simu kwenye begi lake ikiwa imezimwa kitu ambacho ni kosa.

Hata hivyo katika hospitalini hapo Elimtaa Media inakutana na mtu anaye daiwa ni kaimu afisa elimu ambaye anakana kuwa ni afisa elimu, na kuwa anafanyia idara hiyo na Hospitalini hapo yupo kwaajili ya kuw ana mgonjwa wake.

Afisa huyo Anton inadaiwa kuwa ni kaimu afisa elimu alisema kuwa Ofisini kwake kuhusiana na tukio hilo, taarifa hana uhakika kama imefika licha ya yeye kuwepo ofisini.

Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri anakili kuwapo kwa tukio hilo wilayani kwake licha ya yeye kuwa mbali ofisi ambapo anasema kuwa alifika katika hospitali hiyo na kumuona na alimuona  mwanafunzi huyo  akiwa amepigwa na alama za fimbo.

Baadhi ya viongozi waliofika hospitalini hapo na kuzungumza na mwanafunzi huyo wanaeleza hali yake ambapo bada ya kuzungumza na mwanafunzi huyo walieleza kuwa alichapwa na waalimu baada ya kukutwa simu ya mkononikatika begi lake.


Aidha diwani wa kata ya Ramadhani George Sanga anasema kuwa mtoto huyo aliwaeleza kuwa alichangiwa na waalimu sita akiwemo na mkuu wa shule hiyo.

Alisema kuwa mwanafunzi kuadhibiwa akiwa na kosa si tatizo ila tatizo ni waalimu walivyo mwadhibu mwanafunzi huyo kwa kuwa kuwa na simu hairuhusiwi kwa mwanafunzi.

Naye diwanai wa kata ya Mjimwema Abuu Mtamike alisema kuwa kinacho msikitisha ni waalimu kumchangia mwanafunzi mmoja wakike huku waalimu hao wengi wao wakiwa ni wanaume wakati shuleni hapo kulikuwa na mwalimu wa kike.

Hata hivyo baba wa mtoto huyo alisema kuwa taarifa za bindiye kupigwa alizipata kutoka kwa mtoto wake na kufika hospitalini kutoka mkoani Songwe licha ya kuwa wakati akizungumza na Elimtaa Media bado chanzo cha kupigwa kwa mtoto wake alikuwa bado hajakijua.