Wakulima Wazungu wa Zimbabwe kuwalipwa fidia.


Image captionMkulima akitazama uharibifu baada ya uvamizi shambani mwake Harare
Taarifa kutoka Zimbabwe zinasema serikali inafanya mipango ya kuwalipa wakulima wazungu waliopoteza ardhi wakati wa uvamizi ulioungwa mkono na serikali miaka 16 iliyopita.
Shirika la habari la The Bloomberg linasema wizara ya fedha ya Zimbabwe imetoa taarifa ikieleza kuwa wakulima hao watapokea fedha kufidia hasara waliopata ya ardhi na mali.
Waandishi nchini humo wanasema iwapo hatua hiyo itathibitishwa, itakuwa sawa na kwenda kinyume na kauli ya rais Mugabe kupinga malipo yoyote kwa ardhi hiyo.
Mugabe amesisitiza katika siku za nyuma kuwa wakulima hao hawapaswi kulipwa kwasababu ardhi hiyo iliibiwa kutoka kwa Waafrika wakati wa utawala wa mkoloni.
Uvamizi huo ulilenga mashamba ya tumbaku, zao lililouzwa kwa wingi kwa wakati mmoj kutoka Zimbabwe, na hilo likasababisha ukame mkubwa kati nchi hiyo iliyokuwa muuzaji wa pili kwa ukubwa Afrika wa mahindi.
Zimbabwe inajaribu kuurudisha uhusiano na shirika la fedha la kimataifa IMF na taasisi nyengine za fedha duniani.