USAFI WAENDELEA KUHAMASISHWA DAR

MZ1 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Dar es salaam na Halmashauri ya Wilaya ya Ilala wakiwasili eneo la soko la Feri jijini Dar es salaa kujionea hali ya usafi wa soko hilo.
MZ2 
Baadhi ya wahudumu wakiendelea na usafi eneo la soko la Feri jijini Dar es salaa huku Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba na msafara wake wakikagua na kujionea hali ya usafi wa soko hilo.

MZ3 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba (aliyevaa miwani) akishuhudia Majuto Alli Majuto akiendelea na kazi yake ya kukaanga samaki aina ya pweza katika soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam. Vijana wakiendelea kazi ya kukaanga samaki katika soko la Feri katika mazingira ambayo hali ya usafi siyo ya kuridhisha kwa ajili ya kulinda afya ya mlaji.
MZ5 
Kijana Hamisi Misango akimnyanyua samaki aina ya taa ili amuandae tayari kwa kumuuza kwa wateja wanafuata kitoweo katika soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam.
MZ6 
Msafara wa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba wakishuhudia moja ya shimo la maji mchafu ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wa afya ya wananchi wanaofika katika soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam au wale watakaotumia samaki hao kama hawatakuwa wameandaliwa katika hali ya usafi na salama. Lengo ni wananchi wengi wanaofika sokoni hapo ni kununua samaki waweze kuwauzia watu wasoweza kufika sokoni hapo na wengine kwa ajili ya matumizi yao ya nyumbani.
MZ7 
Mama lishe Zainabu Hamad anayefanya shughuli zake za kutoa huduma ya chakula katika soko la Feri zoni 4 kizimba namba 12 akiongea na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba alipotembelea sokoni hapo kwa lengo la kuhamasisha suala la usafi kwa manufaa ya kulinda afya ya wananchi wanatumia huduma hiyo wakiwa sokoni humo.
MZ8 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba na msafara wake wakiwa katika eneo la soko la Kariakaoo kukagua suala la usafi unavyozingatiwa sokoni humo. Licha ya uchafu uliopo katika soko la Kariakoo, wafanyabiashara wa matunda hawachukui tahadhari yeyote ya kulinda afya za walaji wa matunda ambapo wanauza matunda aina ya mananasi bila kuyafunika sa kusababisha inzi kuyazonga zonga matunda hayo kitu ambacho ni hatari kwa suala la usalama wa afya ya malaji.
MZ9 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba akijionea wafanyabiashara wadogo walivyovamia miundombinu ya Mradi wa Mabasi yaendayo kwa kasi katika eneo la Kariakoo jijini Dar es salaam huku mafundi wakiendelea na kazi ya kupaka rangi.
MZ11 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba akitembelea maeneo mbalimbali ya soko la Kariakoo jijini Dar esa salaam. (Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)