TANESCO NUNUENI NGUZO ZA NDANI KUKUZA UCHUMI


 BIDHAA ZA MITI ZINAZO TENGENEZA KIWANDA CHA TANWAT NJOMBE






  KATIBU MKUU WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA, ULEDI MUSSA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI



 MAELEZO KWA BAADHI YA BIDHAA KIWANDANI HAPO

 MATEMBEZI NDANI YA KIWANDA

 MMOJA WA VIONGOZI KATIKA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MARIGHAFI KATIKA KIWANDA CHA TANIWATI AKIONYESHA KIWANDA KINAVYO FANYA KAZI
KATIBU MKUU VIZARA YA WIWANDA NA BIASHARA ULEDI MUSSA (WA NNE KUTOKA KUSHOTO)AKIPOKEA MAELEKEZO KATIKA KIWANDA CHA KUZALISHA BDIDHAA MBALIMBALI ZA MITI KATIKA KIWANDA CHA TANI WATI MKOANI NJOMBE
 KATIBU MKUU WA VIWANDA NA BIASHARA ULEDI MUSSA AKISIKILIZA KWA MAKINI MAELEZO KUTOKA KWA MKURUGENZI WA TANWAT, BRAHM GOSWAM


 MKURUGENZI WA TANGANYIKA WATTLE COMPUNY LTD BRAHM GOSWAM AKITOA KUFAFANUZI WA JAMBO KWA KATIBU MKUU WA VIWANDA NA BIASHARA (HAYUPO PICHANI)



 MENEJA WA UTAWARA NA FEDHA KIWANDANI HAPO EDMUND KINUBI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI 
 MENEJA WA MISITU KIWANDANI HAPO ANTERY KIWALE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
 MILANGO ILIYO TENGENEZA KIWANDANI HAPO

 MWANAMKE KAZINI AKIOPARETI MTAMBO WA KUTENGENEZA MBAO NYEMBAMBA UNAO BANDUA MAGOGO






    
 MENEJA WA UTAWALA NA FEDHA EDMUND KINUBI AKIONYESHA BAADHI YA NGUZO AMBAZO ZINATENGENEZA KIWANDANI HAPO NA KUWA NA UBORA NA KUPELEKWA NCHINI KENYA NA TANESCO IKINUNUA NGUZO KAMA HIZO NJE YA NCHI



KIWANDA CHA UMEME KWA NJE




Sehemu ya mtambo wa kuzalisha umeme ambapo kunazalishwa umeme wa megawat 2 huku wakibakiwa na megawat 1 na kutumia moja

 Baadhi ya bidhaa zinazo tokan ana miti 
Baadhi ya wafanyakazi katika kiwanda cha Tanwat cha mkoani njombe kinachi zalisha nguzo na mbao laini kwaajili ya thamani

Picha ya pamoja kiwandani hapo

**************

VIWANDA vya ndani vimekuwa vikikosa tenda za usambazaji wa huduma mbalimbali kama wazabuki kutojana na tenda hizo kuandaliwa maofisini kwa kusoma makaratasi badara ya kufika katika katika eneo la mzabuni anaye omba tenda.

Hali hiyo imeikuta shilika la umeme Tanzania (Tanesco) ambapo inadaiwa kuacha nguza za umeme za ndani na kununua kwa bei kubwa nje ya nchi huku makampuni ya uzalishaji wa nguzi ya hapa nchini yakiziuza nguzo kama zinazoi nunuliwa nje na Tanesco nchi ya jirani ya Kenya.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea kiwanda kinacho zalisha nguzo za umeme na bidhaa mbali mbali za miti cha Tanganyika Wattle Company (Tanwat) cha Mkoani Njombe kuuza nchini Kenya wakati Tanesco wakinunua nguzo hizo hizo nje ya nchi katibu mkuu wa wiwanda na biashara Uledi Mussa alisema kuwa tenda nyingi zinaamuliwa ofisini bila kufika katika eneo la mtu anaye omba tenda.

Alisema kuwa Tanesco wamekuwa kiwapa tenda watu bila kufika katika eneo la mtu anaye taka tenda na kusema kuwa serikali kama itazingatia kutoa tenda kwa kutembelea eneo la mtu anaye taka tenda wazawa watapata tenda na bidhaa za nchini zatanunuliwa kuliko ilivyo hivi sasa zinanunuliwa za nje ya nchi.

Aliitaka Tanesco kuhakikishe kuwa inanunua nguzo kutoka nchini na na pesa inazo zitoa nje ya nchi kubaki hapa Tanzania na kuoneza kuwa tanesco imekuwa ikitumia bilioni 210 kununua nguzi hizo nje ya nchi kwa bei ya juu wakati nguzi zipo hapa nchini na kuuza kwa bei nafuu.

Aidha aliongeza kuwa kiwanda hicho kinaweza kuzalisha nguzo za kuitosha tanesco, na kusema kuwa ameambiwa kuwa katika kiwanda hicho kunamakampuni matatu yanayo chukua nguzo kiwandani hapo na kuwauzia tanesco makampuni hayo yaliomba tenda na kupewa wakiwa oifisini bili kufika katika eneo lao.

Alisema kuwa anashangaa kuona kuwa mtanzania anakuwa anauzoefu nje ya nchi kuliko ndani ya nchi na kuwa kwa miaka mingi kampuni hiyo imekuwa ikiomba tenda ya kuiuzia Tanesco nguzo lakini wamekuwa wakishindwa.
Aidha kwa upande wake meneja wa misitu Tanwat, Antery Kiwale alisema kuwa miaka ya hapo nyuma kabla hawajaanza kuuza nguzo hizo Kenya walikuwa wanawauzia kwa kiasi kidogo Tanesco na kampeni ya simu ya TTCL na kuwa kwa sasa wamepanda miti mingi ambayo kwa mwaka wanweza kuvuna nguzo 120,000 huki wa kila hikta kukiwa na uwezekano wa kuvina nguzo 800.

Alisema kuwa wamekuwa wakishindwa vigezo vidogo sana katika ushindanishwaji wa tenda na kuwa wanauwezo wa kuihudumia Tanesco, na kusema kuwa anacho jiuliza ni kwanini nguzo zinatoka nje ya nchi wakati zipo zinazo zalishwa hapa nchini na kukidhi vigezo vyoye vinavyo hitajika kama urefu na zilivyo tibiwa.

“Tumekuwa tukishindwa kuchuka tenda hapa nchini kutokanana vigezi vidogo ambavyo tungepewa ushauri tengelrekebisha na kuuza nguzo hizi ambazo zingenunuliwa kwa bei nafuu kuliko wanavyo nunua nje ya nchi,” na kuongeza

“Kuwa serikali juhudi zake za kuhimiza wananchi kupanda miti ya kutosha lakini haivunwi itakuwa haina maana kwa kuwa miti inakomaa harafu haisaidii wananchi,” alisema Kiwale

Hata hivyo meneja wa utawala na fedha, Edmund Kinubi alisema kuwa serikali inatakiwa kurekebisha mfumo wa kodi na kuhakikisha inaweka kodi moja hata kama inakuwa kubwa inajulikana kuwa kuna kodi moja kuliko kuwa na kodi nyingi ambazo wawekezaji wanahangaika nazo na kuacha shunguli za uzalishaji.


Kiwanda cha tani wati ni moja ya viwanda vinavyo toa ajira kwa watanzania wakazi wa Njombe kwa vijana wanao fika hadi 1500 kwa msimu wa kawaida na msimu wa kazi nyingi kufikia vijana 3000, ambao wanaajira za kudumu na vibarua.

IMEANDALIWA NA ELIMTAA MEDIA 0753321191