WENYE MAVUMBA (MAPESA) 50 AFRIKA HAWA HAPA

Forbes wametoa orodha ya watu 50 matajiri zaidi barani Afrika.


Kwa mujibu wa Jarida maarufu la Forbes linalofuatiliwa na watu wengi, Mabilionea wapya wamepungua toka mabilionea 26 mwaka jana hadi 23 mwaka huu. Kudorora kwa bei ya bidhaa katika soko la dunia kumetajwa kuwa sababu ya hali hiyo.













Nafasi ya kwanza imeendelea kushikiliwa na bilionea wa Nigeria, Aliko Dangote mwenye utajiri wa dola bilioni 16.7.Mwenyekiti Mtendaji wa METL, Mohammed Dewji amekamata nafasi ya 21 kwenye orodha hiyo akiwa na utajiri wa dola bilioni 1.1. Dewji anaendelea kuwa tajiri namba moja nchini Tanzania.Rostam Aziz amekamata nafasi ya 25 kwa utajiri wa dola milioni 900 huku Said Salim Bakhresa akikamata nafasi ya 36 kwa kuwa na utajiri wa dola milioni 600