UCHAMBUZI WA MECHI YA TAIFA STARS NA ALGERIA WA HAJI MANARA



Ama hakika wengi waliokuwepo Uwanja wa Taifa  jana waliondoka kwa huzuni sana. Waliondoka kwa huzuni sio sababu timu ya taifa ilifungwa. Laa hasha!! Hawakutegemea kupata matokeo ya sare kwenye mchezo wa kufuzu kucheza kombe la dunia dhidi ya miamba ya soka afrika Algeria.

Tayari kwa kila mmoja mechi ilishaisha hasa baada ya kuongoza kwa goli mbili kwa bila.ila mpira ni mchezo wa makosa.mwisho wa mchezo ikawa huzuni kwetu baada ya waarabu wa kaskazin mwa afrika kusawazisha goli zote mbili....

Mengi yameandikwa na kusemwa na 'mabush coaches"wetu baada ya mpira kwisha na najua yataendelea kusemwa mengi ila mwisho wa siku tumehuzunika pamoja kama Watanzania..

Waswahili hunena"kamba hukatia pabovu"

Nyingi za lawama hivi sasa znaelekezwa kwa kocha Charles Boniface Mkwasa kwa kufanya mabadiliko ya kuwatoa Elias maguli na Mudathir Yahya na kuwaingiza Said Ndemla na Mrisho Ngasa..

Walaumuji wanakosoa kwa kusema hakukuwa na haja ya mabadiliko ya kuwaingiza aina ya wachezaji hao sababu tulishashinda na wao si aina ya wachezaji wanaokaba washambulizi zaidi.



Upande mmoja 'bush coaches'wapo sahihi ila tuangalie kwa nini  mkwasa aliamua kufanya sub zile. Na kiufundi kwa nini Algeria walisawazisha zile goli;

Kwanza mie nakubaliana na haki ya kulalamika kwa 'wakosoaji wetumahiri' ila natofautiana na baadhi ya mitazamo ya baadhi yao kuhusisha siasa za Simba na Yanga katika maamuzi ya mwalimu..hii haipo sawa na lazma ikemewe kwa nguvu zote.

Lau kama Mkwasa angetaka 'kubalance"asingesubiri jioni kufanya hvyo. Yeye ndiyo mwenye uamuzi wa nani acheze na nani aanzie nje..

Angetaka angemuanzisha Ndemla na Ngasa na hakuna 'bush coach' yoyote angeweza kuzuia!

Nina mashaka sana wakosoaji wasiojipa muda wa kutafakari walau kidogo na kushusha lawama tu.tena kwa kutoonyesha heshma japo kidogo kwa kocha na wachezaji wetu waliojitoa sana jana:



Nnachoamini kwa jicho langu la tatu ni kwamba baadh ya wachezaji wetu walishachoka na Mkwasa alihitaji aina ya watu wanaoweza kukaa nao sana mpira au wenye kasi zaid. Wakosoaji wanadhani mbinu ya kujilinda ni kuwa na viungo wakabaji tu. Wasichoelewa delaying tactics ni pamoja na kuwa na viungo wenye uwezo wa kukaa na Mpira.

Naamin mbinu ya Mkwasa ingefanikiwa 'bush coaches' sijui wangeandika nini!

Lau wajina wangu asingezubaa kdogo na kutoa mwanya kwa waalgeria na kisha kufanya uzembe wa kukaba kwa macho kwa mabeki kisha waarabu kutuadhibu.sasa hv tungekuwa tunasema mengine.sababu kabla ya uzembe ule na wakati huo kina ngasa tayari wakiwa ndani.mpira ulikuwa kwenye udhibiti wetu na si kweli kuingia kwa viungo hao ndio kulichangiwa na kupoteza umakini;

Nnaloamin mm baada ya waalgeria kupata goli moja.moyo wa kupigana uwanjani kwa wachezaji wetu ulikuwa umeparalaiz.kama si kufa kabisa..

Na hili si kosa la mwalimu.hyo ndio tofaut ya wao na sisi.
Wao wenye wanaume wanaocheza kandanda uropa na sisi tunaowategemea kina samata na ulimwengu waliopo Congo DRC.
Kocha mkwasa na jeshi lake walijitahidi kwa kadri ya uwezo wao.dak 45_za awali zilikuwa bora kabisa kwetu zkichagizwa na kujituma kupindukia kulikopelekea wachezaji wengi kuchoka na kupelekea sehemu fulan ya kipindi cha pili kupoteza umakini.ila huo ndio uwezo wetu kwa sasa na wenye macho tumeona kipo kitu kwa timu yetu ya taifa.
Najua tulipoteza nafasi nyingi za kuwaadhibu mapema ila nimesema mwanzo mpira ni mchezo wa makosa....

Mwisho ingawa si kwa umuhimu ni BRAVO kwa Mbwana Samata kwa kuyawezesha macho yangu kuona moja ya magoli adimu kwenye dimba la taifa....
 
Fainting kali with driboling ya kileo kisha kutupia kwa style ya penalti tena kwa guu la shetan!!

Bravo star wa nchi hivi sasa...


Wenu 'bush mshabiki"

Haji Manara