Aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Vunjo Augustino Mrema amefungua kesi Mahakama Kuu Moshi, kupinga matokeo ya Uchaguzi yaliyomtangaza James Mbatia wa NCCR-Mageuzi mshindi.
Mbatia alishinda Ubunge katika jimbo hilo kwa jumla ya kura 60,187 aliyemfuata ni Innocent Shirima aliyepata kura 16,617 na Mrema alipata kura 6,416.
Mrema amemtuhumu Mbatia, Mkurugenzi wa Uchaguzi Vunjo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kukiuka baadhi ya taratibu za uchaguzi.
Akiongea na waandishi baada ya kufungua kesi amesema, “nimeamua kufungua kesi kwa sababu nataka haki yangu.”
Ameiomba Mahakama kufuta matokeo ya Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo hilo na kutaka uchaguzi urudiwe.
Kwa mujibu wa Ndugu Mrema, James Mbatia alisambaza karatasi za kupigia kura kabla ya siku ya uchaguzi akitaka wananchi wampigie kura, amesema kuwa Mbatia alisambaza karatasi za kupigia kura mpaka makanisani na kwenye misikiti.
Chanzo: JF