Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo akikata utepe kuzindua Kisima cha maji safi na salama katika kijiji cha Machali A wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma mwishoni mwa juma lililopita.
Na Modewjiblog team, Chamwino.
KIJIJI cha Manchali kilichopo wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, kimekabidhiwa mradi wa dola za Marekani 150,000 wenye lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mradi huo ulikabidhiwa kijiji hicho na Mratibu wa mashirika ya Umoja wa mataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Alvaro Rodriguez.
Mradi huo umelenga kusaidia jamii inayoishi katika kijiji hicho kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mradi huo wa nishati ya jua umelenga kutatrua tatizo la nishati na kufanya matumizi bora ya ardhi na teknolojia ya maji.Mradi huo unasaidia familia 600.
Kwa uzoefu wa Tanzania na maeneo mengine duniani, familia maskini ndizo zinazopigika vibaya na mabadiliko hayo na ndio haizna uwezo wa kukabiliana nayo.
Kwa mradi huo wananchi wa Manchali wanatarajia kukabiliana vilivyo na mabadiliko ya Tabia nchi.
Akizungumza katika kijiji hicho cha Manchali, Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Bi. Awa Dabo alisema kwamba ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi uwezeshaji wananchi kiuchumi ni muhimu sana ili kufanya familia kustawi.
Kisima kilichozinduliwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo.