Rais Magufuli ameanza kuhutubia bunge
-Anasisitiza kutimiza ahadi zake alizoahidi
-Analipongeza jeshi la polisi na Tume ya Uchaguzi kwa kufanikisha zoezi zima la uchaguzi
-Kampongeza sana Zitto Kabwe kwa kutozomea na kutoka nje kama walivyofanya wabunge wengine wa upinzani
-Rais Magufuli anawapongeza marais wastaafu waliomtangulia kwa nzuri walizofanya
-Kasema tumemaliza uchaguzi tukiwa wamoja, hivyo serikali yake itahakikisha inadumisha amani hii kwa gharama yoyote
-Rais amesema wakati wa kampeni, wananchi walitoa malalamiko mengi kama Rushwa,migogoro ya ardhi,kuhodhi maeneo bila kuendelezwa,uvivu, matumizi mabaya ya mali za umma, matatizo ya maji
-Kasema eneo lingine lililolalamikiwa ni Uwepo wa Rushwa TRA na ukwepaji kodi, Tanesco kukata umeme hovyo, watumishi wa maliasili kujihusisha na ujangili
-Mengine yaliyolalamika ni ubovu wa huduma za afya, lugha chafu za waaguzi na tozo za ajabu
==>Mh.Spika nimeamua kuyataja haya ili tujue pakuanzia
-Sehemu nyingine inayolalamikwa ni uhamiaji, pia suala la Elimu ambapo kuna malalamiko ya walimu na huduma mbovu kwa wanafunzi
-Lawama pia zilitolewa katika sekta ya madini ambapo wazawa hawanufaiki,Mizani rushwa imekithiri,Mahakamani haki zinapindishwa, uvuvib haramu, wakulima kutopewa pembejeo za kilimo
-Eneo lingine ni uchakavu wa Reli, kuzorota kwa shirika la ndege
==> Hizi ni baadhi ya kero ambazo nimezitaja ili kwa pamoja tusaidiane kuzitafutia ufumbuzi
Pamoja na kero hizo, kuna mambo mengine ambayo tumejipanga kuyasimamia na kuyatatua. Mambo hayo ni;
1. Kuulinda muungano wetu
2. Kuimarisha mihimili ya Serikali
-Tutahakikisha kuwa mihimili yetu ya Bunge na Mahakama inapata pesa za kutosha ili iweze kufanya kazi zake kwa uhuru
3. Mchakato wa katiba mpya.
-Serikali yangu inatambua kazi kubwa iliyofanywa na watangulizi wetu pamoja na bunge la katiba lililotupatia katiba pendekezwa.Tunaahidi kutimiza wajibu wetu kumalizia kiporo hiki tulichoachiwa
4.Uchumi na matarajio ya wananchi
-Tutaboresha miundo mbinu ili kuinua uchumi. Tumejipanga kuzijenga upya Reli zetu ili kuboost vizuri uchumi wetu
-Tuna gesi na madini,tutahakikisha wananchi wote wananufaika na rasrimali hizi.
5.Ujenzi wa Viwanda
-Serikali ya awamu ya tano itaweka kipaumbele katika ujenzi wa viwanda
-Tutaanza na Viwanda Vilivyopo na kuhakikisha vinafanya kazi
-Waliobinafisishwa viwanda hivyo nawataka waanze kazi mara moja.Wakishindwa tutawanyang'anya.
- Tumejipanga kuhimiza na kushawishi wawekezaji kuwekeza zaidi nchini ili kukuza zaidi uchumi wetu
Sura Ya Viwanda Tunavyotaka Kuviunda
-Sura Ya Kwanza: Ni vile ambavyo malighafi yake itatoka ndani ya nchi
-Sura Ya Pili ya Viwanda hivi ni vile vya kuzalisha vifaa ambavyo vitatumiwa zaidi ndani ya nchi
***Viwanda hivi vitakuwa na uhakika wa soko ndani ya nchi
-Sura Ya Tatu ya Viwanda hivi ni kuzalisha ajira nyingi kwa watanzania
6. Kilimo, Mifugo na Uvuvi
-Tutaziangalia sekta hizi kwa mtazamo wa kibiashara ili kukuza viwanda vyetu.
-Tutahakikisha wavuvi hawavamiwi na majambazi
-Tutafuta kodi za wakulima ambazo hazina ulazima
-Wanachi hawatanyang'anywa ardhi zao kiubabe
7.Umasiki na Ajira
-Nakiri,pengo la wenye nacho na wasio nacho linazidi kuwa kubwa.
-Tumejipanga kupunguza umasikini na kukuza ajira kwa kutilia mkazo uanzishwaji wa viwanda, uvuvi, mifugo na kilimo kama nilivyosema
-Tumejipanga pia kuwawezesha vijana kwa kuwaandaa kielimu na kiujuzi
-Tutahakikisha vyuo vyetu vinawaandaa vijana kiufundi
-Tutawapa vijana mitaji ya kuanzisha makampuni kulingana na fani zao
-Vijana wataanzisha saccoss zao na watatakiwa kujiunga na mifuko ya jamii
==> Makundi maalumu ya Bodaboda,mamalishe na Machinga
- Ushuru usio wa lazima kwa machinga, mama lishe tutaufuta
-Nawataka viongozi wote wa halimashauri wasiwanyanyase watu hawa kwa namna yoyote ile na sitawavumila.
8. Afya
-Tutaimarisha huduma za afya pale zilipo na kuzianzisha pale ambapo hazipo
-Tutawapatia mafunzo watumishi wake ndani na nchi
-Tutawapatia vifaa vya kutosha ili kuondoa ulazima wa watu kutibiwa nje
-Tutaongeza bajeti ya wiraza ya afya.
9. Elimu
-Tutaongeza mkazo katika masomo ya sayansi
-Tutahakikisha vifaa na maabara vinaongezwa
-Kuanzia Mwakani elimu ya shule ya msingi hadi kidato cha nne ni Bure na hakutakuwa na michango.
-Wanafunzi wa Vyuo watapata mikopo kwa wakati
-Matatizo ya walimu yatatiliwa mkazo
10. Maji
-Tutaongeza upatikanaji wa maji kwa asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mijini.
-Hatutaki akina mama kubeba ndoo kichwani.Tutaboresha miundo mbinu ya maji
11.Umeme
-Tutakamilisha miradi iliyopo na mingine mipya itajengwa ili kuhakikisha upatikanaji wa umeme kwa kiwango kikubwa.
-Pale mtera kuna hujuma, watu wanafungulia maji ili yamwagike hovyo wauze mafuta. Naahidi kupambana Nao.
12.Madawa ya Kulevya.
-Tunaahidi kuusaka kwa gharama zozote mtandao wa wauza madawa ya kulevyo.
-Tutashughulika na wakubwa sio vidagaa na hatutawaogopa na mungu anisaidie
13. Rushwa na Ufisadi.
-Nachukia sana Rushwa na ufisadi
-CCM tumejengwa katika imani ya kukataa Rushwa na Ufisadi, japo sina imani sana kama wanachama wa sasa hawatoi na kupokea rushwa.
-Wananchi wamechoka sana na Rushwa na hawako tayari kuvumilia UPUUZI wa serikali kuwavumilia mafisadi na wala Rushwa
-Dawa ya jipu ni KULITUMBUA......Nimejipa hii kazi ya kuyatumbua haya majipu
-Nafahamu ugumu wa vita niliyoamua kupambana nayo maana Rushwa hutendwa na viongozi wakubwa wa nchi, lakini naamini wananchi wataniunga mkono katika mapambano haya ya Rushwa na Ufisadi.
-Ili kulitatua tatizo hili, nimedhamiria kuanzisha mahakama ya Rushwa na Mafisadi
- Kiongozi yeyote ntakaye mteua na kujihusisha na Rushwa NITAMTIMUA MARA MOJA na hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa
14. Baraza dogo la Mawaziri
-Nimejipanga kuunda serikali ndogo itakayojikta kuwatumika wananchi.
-Watumishi wavivu, wazembe hawatakuwa na nafasi ndani ya serikali yangu
-Tumewavumilia vya kutosha.....Sasa Inatosha, hatutawafumbia macho
-Pamoja na hilo, lakini pia tumejipanga kupunguza kodi ya wafanyakazi na kuboresha mishahara yao.
15.Ukusanyaji wa Mapato na kubana matumizi
-Tumejipanga kushughulika na wakwepa kodi wote ili kukuza uchumi wetu
-Safari zote za nje ya nchi tutazifuta na tumeshaanza.
-Hata kama ikitokea kiongozi akasafiri hatutaruhusu aambatane na msafara mkubwa usio na ulazima.
-Kuna watu hapa wameshasafiri nje ya nchi mara nyingi zaidi kuliko walivyosafiri kwenda kwa wazazi wao
-Takwimu nilizonazo ni kuwa kwa mwaka huu wa pesa zaidi ya bilioni 356.324 zilitumika kwa safari za nje.Huu ni ubadhilifu wa mali za umma
-Warsha,semina na makongamano yote tutayafuta
-Sheria ya manunuzi nayo ni mdudu mbaya. kalamu ya 1000 hununuliwa kwa sh.10,000. Sheria hii lazima tuibadilishe
-Magari ya gharama kwa viongozi waandamizi wa serikali yatadhibitiwa
****Vipaumbele Vya Serikali Yangu
1.Kupunguza urasmu
2.Kubana matumizi
3.Kurejesha nidham ya serikali na utumishi wa serikali
4.Kupunguza ukubwa wa baraza la serikali
5.Tutaongeza nidham ya matumi serikalini
==> Rais Magufuli amehitimisha Hotuba yake na kutangaza kulifungua Rasmi Bunge la 11
-Baada ya Rais Magufuli kumaliza Hotuba yake, Waziri mkuu ameitwa kwa ajili ya kutoa hoja ya kuahirisha kikao cha kwanza cha bunge la 11
-Waziri Mkuu ametoa hoja ya kuliahirisha Bunge hili la 11 hadi tarehe 26 Jaruary 2016