Showing posts with label Bungeni. Show all posts
Showing posts with label Bungeni. Show all posts
BARAZA LA MAWAZIRI VIVURI HILI HAPA

BARAZA LA MAWAZIRI VIVURI HILI HAPA

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani  Freeman Mbowe.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Freeman Mbowe.
Hatimaye, Kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe ametangaza baraza lake la mawaziri kivuli leo bungeni mjini Dodoma.
Aidha, Mbowe, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chadema ametaja baraza lake ambalo litakuwa na lengo la kuishinikiza serikali ya Rais Magufuli kutimiza kile alichoahidi kwa Watanzania.
Baraza hilo la Mawaziri litakuwa na kazi kubwa ya kuendana na kauli Mbiu ya Chama cha Mapinduzi ya Hapa Kazi tu katika utekelezaji wa majukumu yake.
Baraza zima la Kambi rasmi ya Upinzani   ni kama ifuatavyo;
1.Wizara ya Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.
Mawaziri – Jaffar Michael
Naibu Waziri – Joseph Nkundi na Ruth Mollel
2.Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
Waziri – Ali Saleh Abdalla
Naibu Waziri – Pauline Gekul
3.Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu
Waziri – Esther Bulaya
Naibu – Yusuph Makame na Maftah Abdalla
4.Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Waziri – Magdalena Sakaaya
Naibu Waziri – Emmaculate Swari
5.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri-Inj. James Mbatia
Naibu Waziri Willy Kombucha
6.Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri – Halima Mdee
Naibu Waziri – David Silinde
7.Wizara ya Nishati na Madini
Waziri – John Mnyika
Naibu Waziri – John Heche
8.Wizara ya Katiba na Sheria
Waziri – Tundu Lissu
Naibu Waziri Abdalla Mtolela
9.Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Waziri – Peter Msigwa
Naibu Waziri – Riziki Shaghal
10.Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri – Juma Omari
Naibu Waziri Mwita Waitara
11.Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri – Godbless Lema
Naibu Waziri Masoud Abdalla
12.Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri – Wilfred Lwakatare
Naibu Waziri – Salum Mgoso
13.Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri Esther Matiko
Naibu Waziri– Cecilia Pareso
14.Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri Anthony Komu
Naibu Waziri Cecil Mwambe
15.Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi
Waziri – Suzan Lyimo
Naibu Waziri Dkt. Ali Suleiman Yusuph
16.Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Waziri – Dkt. Godwin Mollel
Naibu Waziri Zubeda Sakul
17.Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo
Waziri – Joseph Mbilinyi
Naibu Waziri – Devotha Minja
18.Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Waziri – Hamidu Hassan
Naibu Waziri– Peter Lijualikali


Mbunge Jesca Kishoa kayasema haya baada ya kukamilisha adhabu ya kuwa nje ya Bungeโ€ฆ(+Audio)

Mbunge Jesca Kishoa kayasema haya baada ya kukamilisha adhabu ya kuwa nje ya Bunge…(+Audio)

Feb 4 2016 Mbunge wa viti maalum CHADEMA Jimbo la Iramba Magharibi Jesca Kishoa aliingia kwenye headline baada ya kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge vilivyo salia baada ya kukataa kufuta kauli yake ya kumtuhumu Waziri wa Katiba na Sheria DkHarrison Mwakyembe.
Leo amekamilisha siku ya pili ya adhabu yake, kama haukuwa karibu na mimi kwenyeAmplifaya ya Cloudsfm nimekusogezea na hapa.
Bonyeza Play kusikiliza
by Millardayo
TAMKO LA SERIKALI YA TANZANIA KIFO CHA MWANAFUNZI HUKO INDIA HILI HAPA

TAMKO LA SERIKALI YA TANZANIA KIFO CHA MWANAFUNZI HUKO INDIA HILI HAPA



Waziri Mahiga ametoa ufafanuzi huo leo bungeni, na kuthibitisha ni kweli wanafunzi hao wamefanyiwa vitendo hivyo, ambavyo watanzania walikuwa wanavisikia bila kuwa na taarifa rasmi.
“Wananchi wa India walichoma gari lake, na punde kidogo gari lingine lilifuata likiwa na wanafunzi wanne watanzania, mmoja msichana na watatu wavulana, walilisimamisha lile gari na kuwavuta wale wanafunzi nje, na wakamchukua yule msichana na kumvua nguo na kuanza kumtembeza barabarani uchi, wale wavulana walipigwa na gari lao lilichomwa, katika gari lile kulikuwa na simu zao na documents mbali mbali nazo ziliteketea”, alisema waziri Mahiga.

Waziri Mahiga aliendelea kwa kusema kuwa baada ya hapo askari wa India walifika lakini hawakuonyesha ushirikiano wa kutosha, lakini wanafunzi hao walipelekwa hospitali na kupatiwa matibabu ya majeraha waliyokuwa nayo, lakini walilazimika kuondoka mapema kwa kuwa hawakuwa na pesa.

“Baada ya hapo ubalozi wetu wa India uliandika dokezo la kidiplomasia kwa serikali ya India, ikilaani kitendo hicho na kuitaka serikali ya india ichukue hatua za kisheria na haraka katika kupeleleza kufuatia matukio hayo, na waziri wa mambo ya nchi za nje wa India, alitoa taarifa rasmi kule New Delhi,kwanza kuomba radhi kwa Tanzania na watanzania walioko India kwa kitendo hicho kilichotokea, akaagiza serikali yake ichukue hatua za kisheria na kupeleleza na kukamata wale waliohusika, na wote sasa wamekamatwa na wamepelekwa mahakamani”, alisema Waziri Mahiga.

Pamoja na Hayo Waziri Mahiga alisema serikali India iliagiza kwamba wanafunzi wa Tanzania wapewe ulinzi maalum kule wanakoishi na kusindikizwa pale wanapokwenda masomoni au madarasani , na tatu serikali ya India ilimtaka balozi wetu afuatane na maafisa waandammizi wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya India mjini Bangalow, ili kukutana na wanafunzi wa Tanzania na wengine wa Afrika, na kuweka mahusiano mazuri kati ya wananfunzi na wenyeji katika mji huo.

Pia Waziri Mahiga alitoa taarifa rasmi juu ya kifo cha mwanafunzi mwingine Mtanzania nchini humo, na kusema mwanafunzi huyo hakufariki kwenye tukio hilo la uvamizi, bali alipata ajali ya pikipiki iliyosababisha kifo chake.

“Nilielezwa kwamba kuna mwanafunzi mmoja ambaye amefariki karibu na maeneo hayo hayo , taarifa za awali zilikuwa zinatatanisha wakadhani kifo hicho kilitokana na tukio hilo la kuvamiwa wanafunzi wetu, lakini si kweli, mwanafunzi huyo mtanzania alikuwa anaendesha piki piki bila kofia, akaenda kugonga nguzo ya taa na kufariki pale pale, ubalozi wetu unashughulikia mazishi na mwili wake utarudishwa Tanzania mapema iwezekanavyo.

Tukio hilo limeingia siku ya tatu sasa tangu kutokea kwake nchini India, ambapo kumeibuka hisia tofauti tofauti miongoni mwa watanzania, na kuwatia hofu wanafunzi wanaosoma nchini humo.

HII NDO KAULI YA ZITO KABWE MALA BAADA YA HALIMA MDEE KUTEULIWA KUWA Waziri Kivuli Fedha na Mipango



Kategori

Kategori