UTOJIA WA TAARIFA SAHIHI
Baada ya kukamilika kwa uchunguzi uliofanywa na wataalamu wa TEHAMA wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na wale wa CHADEMA,Tume ya Taifa ya Uchaguzi inavisihi vyama vya siasa kuepuka na kuacha kutoa taarifa za upotoshaji kwa kigezo cha kutaka kuonekana vipo makini katika ufuatiliaji na utoaji taarifa.
Kitendo cha kusema na kujiaminisha kuwa unachosema ni sahihi ni kitendo cha kuonesha kutoaminika pale inapodhihirika ulichosema siyo sahihi ni uwongo na upotoshaji mkubwa.
Aidha CHADEMA ni vyema wakawaelimisha mashabiki, wafuasi na wananchama wao kufuata taratibu za mawasiliano na kuepuka kusambaza taarifa za propaganda katika mitandao ya Kijamii ili kuepusha mhemko miongozi mwa watu hasa wakati huu ambapo joto la kisiasa nchini liko juu.
Vile vile kwa kuwa uchunguzi wa kina umeshafanyika na kubaini kuwa kanzidata ya MM integrated steel mills haina uhusiano wowote na ile ya Tume ya Taifa ya uchaguzi,Tume inakitaka CHADEMA kuhakikisha kuwa usambazaji wa picha za BVR kits ambazo zilitumika kuandikisha Wapiga Kura zilizosambazwa na maafisa wao waliokuwa katika zoezi hili katika mitandao ya kijamii zinasitishwa mara moja ili kuepuka kuendelea kuupotosha umma kuhusiana na tuhuma zisizokuwa na ukweli
Tume inapenda kusisitiza kuwa taarifa zote zinazotolewa kwa umma lazima zithibitishwe pasipo shaka ili kuondoa mkanganyiko katika jamii na kuepusha wananchi kuchukua hatua ambazo zinaweza kuleta uvunjifu wa Amani.
Kwa kuwa Uchunguzi wa kina umeshafanyika na kubaini kuwa vifaa vilivyokuwa vinatumika havina uhusiano wowote na BVR kit za Tume ya Taifa ya uchaguzi,Tume inalitaka gazeti la NIPASHE ambalo limekuwa linaripoti kuwa kuna BVR bandia (fake) zimekamatwa waombe radhi kwa kuupotoshwa umma kwa kuandika taarifa sahihi kuhusiana na kile kilichoonekana katika kiwanda hicho badala ya taarifa walizoandika kupitia gazeti la Nipashe toleo na 0578632 la tarehe 10,oktoba 2015.
Kwa kumalizia, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kusisitiza kuwa Amani na mustakabali wa nchi hii uko katika matendo na maamuzi tutakayoyafanya leo. Hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa kila jambo linalijitokeza linapewa tahadhari na umakini wa kutosha ili tusiharibu Amani na Mshikamano tulionao hivi sasa.
Imetolewa na
Kailima R. Kombwey
MKURUGENZI WA UCHAGUZI