Kama ni mtumiaji wa simu za Android (kama mimi) lazima umekwisha kutana na jambo hili. Mara kwa mara simu yako itakupa ujumbe kuwa imejaa. Kinachosababsha simu yako kujaa mapema si simu bali ni program (applications) unazopakua na kutumia pia maudhui kama vile picha, muziki na video.
Je unawezje kuongeza nafasi kwenye simu yako ya Android? Tutatumia mfano wa Huawei Y360. Sababu ya kutumia aina hii ya simu kama mfano ni kwa vile inaaminika na kupendwa na watu wengi, japo ni simu mpya hapa nchini lakini wengi wanazipenda na wanaendelea kuzipenda. Mara kwa mara nikitembelea maduka ya Tigo (zinakouzwa kwa shilingi 160,000 pekee) hukuta foleni za watu na wahusika huripoti kuwa ndizo habari ya mjini kwa sasa.
Jinsi ya kuongeza nafasi kwenye simu yako ya Huawei Y360
Futa programs ambazo huzihitaji. Nenda Settings >> All (Juu kulia) >> Apps kisha futa program ambazo huzitumii.
‘Clear App Cache’ Nenda Settings >> All (Juu kulia) >> Apps, kisha chagua program ambazo zinachukua nafasi nyingi (Mara nyingi huwa Instagram na Whatsapp) kisha bonyeza mahali palikoandikwa Clear Cache.
Hamishia programu zako kwenye memory card. Huawei Y360 huja na internal memory ya 4GB ila unaweza kuweka memory card hadi ya 32GB. Kuhamishia program zako kwenye memory card kutasaidia sana kuongeza nafasi kwenye simu yako.
Tumia Master cleaner. Huawei y360 huja na program maalumu iitwayo Master Cleaner. Hii itakusaidia kudelete mafaili ambayo huyahitaji kwenye simu yako na kukuongezea nafasi zaidi