Tokea mwaka 1982, serikali ya Senegali imekuwa ikipambana na Kundi la Movement of Democratic Forces of Casamance (MFDC), ambalo linapigania haki ya eneo la Casamance kujitenga, baada ya serikali kuu kushindwa kuzisimamia rasilimali za eneo hilo kwa usawa. Hizi ni harakati ambazo zimeshapoteza maisha ya Wasenegali wengi, na kwa bahati nzuri makubaliano ya kusitisha mapigano (Unilateral Ceasefire) yalifikiwa Mei 1, 2014. Pamoja na hilo, watu wengi wa eneo hilo bado wanahitaji msaada wa hali na mali. Hivyo basi, Waafrika walikutana mjini Tuebingen, Ujerumani na kufanya tamasha, ambalo lilikuwa na kusudio la kuelimisha na kukusanya pesa kwa ajili wa wahanga wa vita hivi. Baadhi ya picha kama zilivyonaswa na Thehabari zinaonekana hapo chini.
Warembo kutoka Afrika pia walikuwepo, na walifurahi.
Taarifa zaidi za maswahibu ya Casamance yanapatikana hapa