Kampuni ya ConnectMoja Technologies Wamezindua tovuti mpya iitwayo Mavazi Store (www.mavazi.co.tz) ambayo inajumuisha Mkusanyiko wa maduka
mbalimbali ya mavazi ya aina zote mtandaoni.
Kwa Mujibu wa Meneja Chapa ambaye pia ni Ambasador
wa Mavazi Store bwana Steve
Seducter mfumo huu wa kisasa
umelenga Kuondoa kero ya kutafuta bidhaa
mbalimbali zinazohusiana na Urembo pamoja na Mavazi, pia kuwaokolea muda wateja
kwa kuunganisha maduka Mengi zaidi kupitia tovuti hii ya www.mavazi.co.tz . Mtu
yeyote mwenye simu ya kiganjani au kupitia katika kompyuta yake ataweza
kutembelea Tovuti hii na kuona biashara zilizosajiliwa pamoja na Bidhaaa
wanazouza. Hii itamuwezesha kuchagua na
kuwasiliana na duka husika Moja kwa moja alipo (Delivery),
Muonekano wa Tovuti ya MavaziStore (www.mavazi.co.tz)
Pamoja na mengine Mtafiti wa Masoko na
ukuaji wa biashara Bwana Fred Crich
alifafanua kwamba kwa Sasa
ConnectMoja Technologies imejikita kusaidia ukuaji wa biashara mbalimbali za
kitanzania, na kuhakikisha kwamba Maendeleo yanayotokea katika Dunia hasa
kupitia teknolojia yanaipa Manufaa pia jamii yetu ya Kitanzania. Crich
Ameongeza kwamba Kwa Kampuni inatoa Ofa
kwa wamiliki wa maduka kutangaza katika Tovuti hii Bure kwa Mwezi Mmoja ili kuwafikia zaidi wateja walio wengi. Ili Kutangaza
Nasi Tembelea http://mavazi.co.tz/advertise/ au Wasiliana nasi kwa Simu 0777880007 au 0714215 600 :
Office: Oysterbay – Dar free
Market Mall (GL14)
Imetolewa na Kitengo Cha Masoko – ConnectMoja Technologies
Limited