ifa ya Tanzania Taifa Stars Charles Borniface Mkwasaameamua kufanya maamuzi ya ziada baada ya klabu za Azam FC na Yangakutowaruhusu wachezaji wake kujiunga na kambi ya Taifa Stars August 9 na badala yake kuendelea na maandalizi yao ya mchezo wa Ngao ya Hisani utakaopigwa August 22.
Mkwasa amelazimika kuita wachezaji wapya kumi ili kuendelea na program yake ya mazoezi kama kawaida hivyo hao ambao hawajaruhusiwa kujiunga atawaangalia katika mechi ya Ngao ya Hisani kwani hawezi kumchukua mchezaji ambae hayuko vizuri na labda ana majeruhi ndio maana aliitisha kambi ya siku kadhaa kablaa ya wachezaji kurejea katika vilabu vyao
Mkwasa alitangaza kikosi cha timu ya taifa Ijumaa ya August 7 hivyo wachezaji wote wanaocheza Ligi ya ndani walitakiwa kuripoti siku ya Jumapili ya August 9.
Wachezaji walioongezwa kikosini ni golikipa Saidi Mohamed, Vicent Andrew, kutokaMtibwa Sugar, Mohamed Hussein (Tshabalala) na Ibrahim Ajib, kutoka Simba,Hamis Ally na Juma Mbwana kutoka KMKM, Tumba Swed kutoka Coast Union,Samwel Kamuntu kutoka JKT Ruvu na Ibrahim Hilka kutoka klabu ya Zima moto ya Visiwani Zanzibar sambamba na golikipa wa Tanzania Prisons Mohamed Yusuphambae bado hajawasili kikosini.