Wayne Rooney akibadilishana mawazo na Louis van Gaal wakati wa mazoezi ya kujifua.(Picha na Getty Images).
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Kocha wa Manchester United, Louis Van Gaal amesema anaanza kuingiwa na hofu ya kibarua chake baada ya sare ya bila kufungana dhidi ya PSV Eindhoven ya Uholanzi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Van Gaal amesema imeingiwa na hofu hiyo kutokana na mashabiki wa timu hiyo kutaka kupata magoli mengi jambo ambalo limekuwa ngumu kwa wachezaji wao hali inayopelekea mashabiki kuanza kuwa wakiimba nyimbo kuwataka wachezaji wafunge magoli.
“Ndiyo nakuwa na hofu ya kibarua lakini jambo la kufunga magoli huwa halitabiriki tunaweza kuwa tunapata magoli na muda mwingine tusiyapate,” amesema Van Gaal.
Akizungumza hali ya mchezo wa jana dhidi ya PSV kwa wachezaji wake kushindwa kupenya mabeki wa PSV na kufunga, Van Gaal amesema “Wao pia ni binadamu inakuwa inatokea kushindwa na yawezekana kukawa na tatizo lakini hawezi jua.
” Kipindi cha kwanza tumecheza vizuri na kutengeneza nafasi lakini hatukufanikiwa na hata kipindi cha pili nimefanya mabadiliko lakini hakuna kilichobadilika”
Kocha huyo tangu kuanza kwa msimu huu amekuwa akizungumza na watu waliokaribu na timu hiyo kutokana na aina yake ya ufundishaji wa kupiga pasi nyingi lakini kufunga magoli kuwa ngumu na mashabiki wa Manchester United wao wakitaka magoli zaidi hivyo kumpa wakati mgumu kocha huyo mdachi.