WATANO FAMILIA MOJA WAFA

WATU watano wa kazi wa Ludewa kutoka familia moja wamefariki dunia katika ajali ya gari ambayo iliacha njia na kutumbukia mtoni akiwemo mwanafunzi wa chuo cha uuguzi Lugalawa wilayani Ludewa.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Wilbroad Mtafungwa akizungumza na waandishi Agosti 2015
Akizungumza na waandishi wa habari mkoa wa Njombe Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Wilbrod  Mtafungwa (Pichani) alisema kuwa watu watano wa familia moja walifariki duni katika ajali ya Gari yenye usajili T 613 AKA  iliyotokea katika mto baada ya gari hiyo kuacha njia.

Mtafungwa alisema kuwa marehemu walikuwa wakisafiri kutoka Lugalawa na kuelekea Shaulimoyo gari waliyo kuwa wakisafiria kutokana na mwendo kasi wa gari hiyo dereva Halon Haule alishidwa kuimudu gali hiyo na kuingiza mtoni.

Aliwataja marehemu katika ajali hiyo kuwa ni pamoja na dereva Haule, Winslaus mtweve (40) Upendo Malawa (29), Editor Mtega, (35) Pascko Mlwilo, (22) Mwanafunzi wa chuo cha uuguzi Lugalawa.

Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva huyo na kusababisha vifo vya wanafamili hao watano ambao walifariki papo hapo.

Alisema kuwa kasi ya dereva huyo alishindwa kulimudu gali hiyo na kusababisha kuingiza katika korongo lililopo katika eneo la Lugalawa ambapo chini yake kulikuwa na mto.

Aliongeza kuwa katika tukio lingine limetokea katika kijiji cha Malimbuli, Kata ya Manguti, wilaya Makete afisa mtendaji wa Alex Josephat, kijiji aligundua kuuwawa kwa kuungua moto mtoto Joshua Seth (2)mkazi wa kijiji hicho.

Alisema kuwa marehemu aliungua kwa moto mpaka kufa akiwa amelala nyumbani kwake na huku akituhumiwa Magreth Msigwa ambaye alikimbia mara baada ya tukio hilo.

Alisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni kuwapo kwa wivu wa kimapenzi baina ya mtuhumiwa na marehemu kwa kuhisi kuwa kuna uhusiano wa kimapenzi baina ya  Mama wa marehemu na mume wa mtuhumiwa.


Aidha jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kumkamata mtuhumiwa na kujibu mashiutaka yanayo mkabili.