SERIKARI imeomba kuhakikisha inapo fanya ujenzi wa barabara na miundombinu yake kuhakikisha maji ya mvua yanaelekezwa katika ardhi na sio katika maporomoko ya miyo ili kuendeleza kuwa na chemchemu kwa mda mrefu.
Wito huo umetolewa katika siku maalumu ya shirika linalofanya kazi ya Maendeleo kwa jamii kwa kuchima visima vya mkopo na kutoa elimu kwa vijana Mkoani Njombe la Shipo na Meneja wake, Edward Oygen.
Amesema kuwa serikali inapo tengeneza barabara na wananchi wanapo jenga nyumba zao wamekuwa wakielekeza maji katika mito na makorongo ambako kitaalamu wanapoteza maji na kuto kuwapo kwa visima endelevu.
Amesema kuwa kwa wataalamu wa barabara wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanapo tengeneza barabara kuelekeza mifereji ya maji katika maeneo ya ardhi na sio katoka mapolomoko ya mito kitu kitakacho sababisha kuwapo kwa maji chini ya ardhi.
Oygen alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa vijana mbalimbali Mkoani Njombe juu ya Ufundi wa visima, kilimo cha umwagiliaji, na elimu juu ya uvunaji wa maji ya mvua.
Ameongeza kuwa kwa siku hiyo ya jana ni siku ya kutoa elimu kwa jamii kwa ujumla na maonyesho ya shughuli wanazi zifanye kwa ujumla.
Kwa upande wa wataalamu walio shiriki katika maonyeshi hayo wamefundisha mambo mbalimbali ya uvunaji wa maji, uvutaji wa maji kwa njia rahisi, na umwagiliaji kwa nyia ya matone.