Rais wa Uturuki aitisha uchaguzi mkuu


Rais Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ametangaza uchaguzi mkuu. Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mwezi Novemba mosi mwaka huu.
Tangazo hilo linatukia baada chama chake Bwana Erdogan cha AK kupoteza wingi wa wabunge katika uchaguzi wa ubunge uliofanyika mwezi Juni.
Tatizo lingine lililopelekea kuitishwa kwa uchaguzi mkuu ni baada ya mazungumzo ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kusambaratika.
Rais Erdogan anapinga madai kuwa anahujumu juhudi za uundaji wa umoja wa kitaifa na badala yake akaamua kuitisha uchaguzi mkuu.
Sasa atamtaka waziri mkuu, Ahmet Davutoglu, kuunda serikali ya muda ambayo itaendesha maswala ya serikali hadi uchaguzi huo mkuu utakapofanyika mwezi Novemba.