MH. TEMBA, JOKATE KIDOTI KUTOKA NA FUNDI..ITAKUWA BALAA

Mwanamuziki anayekimbiza kwenye game la muziki wa Kibongo, Aman Temba ‘Mh. Temba’.Boniphace Ngumije
MWANAMUZIKI anayekimbiza kwenye game la muziki wa Kibongo, Aman Temba ‘Mh. Temba’ siku si nyingi anategemea kuibuka na ngoma inayoitwa Fundi, aliyoifanyia katika Studio ya Mj Records chini ya produza Marco Chali na kumshirikisha mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate.
Mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate.Mh. Temba aliitonya Showbiz kuwa, wimbo huo wenye mahadhi ya kimalavidavi ilikuwa autambulishe mapema wiki hii lakini menejimenti yake imembania na kumtaka asubiri kwanza wamalize kushuti video.
“Jokate kafanya kweli kwenye hiyo ngoma, mashabiki wasubirie kitu kizuri maana niko katika hatua za mwisho za kufanya video kwa Adam Juma, soon ikikamilika kama manejimenti ilivyotaka nitaiachie kwenye media,” alisema Temba.