Mfumo wa Chadema ni upi?!

Siku za hivi karibuni neno mfumo limekua maarufu sana, hivi huwa lina maana gani hasa? Je chadema hawana mfumo? Na kama wanao ni mzuri au mbaya? Umepimwaje? 


Aliyeanzisha chama ni Edwin Mtei na ndiyo mwasisi wa Chadema na ndio Mwenyekiti wa kwanza wa Chama hicho,

Mwenyekiti aliyefuata ni marehemu Bob Makani ambae alimuoa dada wa Mtei, na Mwenyekiti wa sasa Kamuoa mtoto wa Mtei ambae ni mwasisi na mwenyekiti wa kwanza wa chadema, sababu ya Zitto Zubeir Kabwe kutoka Chadema si aliutaka uenyekiti au siyo?

Kilicho mtoa Dr. Wilbroad Slaa kwenye ugombea si ni huo huo mfumo ama nini? sasa napata shida huu wimbo wenu unaoimbwa kila siku wa mfumo!
Watu wanachaguliwa kwa kura za Maoni halafu wanasimamishwa watu ambao hata majina yao hayakuingia kwenye Mchakato wa kupigiwa kura za maoni!

Watus walioshika Nafasi ya 3 na ya 4 kwenye Mchakato wa Kutafuta Wagombea katika kura za maoni nao wamechaguliwa na kukata walioshinda Huu Mfumo ni kitu gani hasa ambacho hawa Jamaa pioneers wa Mabadiliko ambayo ukiwauliza Mabadiliko gani mnayoyataka hawayajui!

Mnatakawa kuubadilisha Mfumo je mnataka kuleta Mfumo upi? Mfumo wa Mwenyekiti kumpitisha Demu wake awe Mgombea wa Ubunge viti Maalum bila Kupingwa? Ama nini?

Huko Mara wanasema wamepambana mno kukijenga chama wakamchagua Mtu ambae walikuwa na Imani nae wanashangaa Kuletewa jina la Mtu ambae hawakumchagua kwenye Kura zao za Maoni, Mtu ambae amejiunga na Chama Wiki mbili zilizopita tu??

Mfumo ni nini hasa?