Kilicho sababisha Makete Uchaguzi kura za maoni urudiwe hiki hapa



CHAMA Cha Mapinduzi CCM wilaya ya makete Mkoani Njombe ambacho Kesho kinarudia uchaguzi wake wa kura za maoni, kimejipanga kwa kuweka wasimamizi watatu katika kila kituo cha uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha kuwa mapungufu yaliyo jitokeza kuto jitokeza tena.

Akizungumza na Elimtaa Mkoani Njombe kwa njia ya simu katibu wa chama hicho wilaya ya Makete Salum Chone  alisema kuwa chama hicho kimejipanga kuhakikisha kuwa makosa yaliyo jitokeza katika kura za maoni hayajitokezi mapema.

Alisema kuwa chama hicho kwa wilaya ya Makete kulitokea makosa ya wagombea kutangaza matokeo kabla ya kutangazwa na Mkurugenzi wa uchaguzi wa wilaya hiyo.

Alisema kuwa kueopusha matokeo yatakayo sababisha malalamiko ni kuhakikisha kuwa kila kituo cha uchaguzi kunakuwa na wasimamizi watatu.

Choneuchaguzi uliopita kulikuwa na shida ya wasimamizi kuto kuwa na maadili na kutoa matokeo ya wagombea kabla ya kufika kwa Mkurugenzi wa uchaguzi.

“Katika uchaguzi uliopita kulikuwa na malalamiko kutoka kwa wagombea kuwa matokeo yalitolewa kabla ya Mkurugenzi wa uchaguzi ndio malalamiko makubwa yaliyo sababisha matokeo kupingwa katika jimbo hili,” alisema Chone

Alisema kuwa kuna baadhi ya wagombea walishiriki kubadilisha matokeo kwa kushirikiana na mawakala wa uchaguzi na kusababisha wengine kulalamika kutokana na kuto kuw ana imani na baadhi ya mawakala wa uchaguzi.

“Kuna baadhi ya wagombea walishirikiana na mawakala kubadilisha matokeo ya uchaguzi na kitu hichi pia kilisababisha kutokea kwa malalamiko,” Chone

Kwa upandewake katibu wa CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpagike alisema kuwa anaelekea huko na siku ya Kesho wakati uchaguzi unaendelea akakuwa wilayani Makete kwaajili ya uchaguzi huo.

Matokeo ya awali katika uchaguzi wa kwanza jimbo hilo kulikuwa na wagombea watano walliokuwa waking’ang’a kuchaguliwa na wananchi kuwakilicha chama chao katika uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu mbunge wa jimbo hilo Binilith Mahenge alipata kura 8534 Norman Sigala kura 8211, Bonic Muhami 500, Fabianus Mkingwa kura 466 na Lufunyo Rafael 226.

Related Posts