Watu Wawili Kastory Msigwa Mwenye Umri Wa Miaka 24 Na Lukha Mgaya Mwenye Umri Wa Miaka 23 Wanaosadikika Kuwa Ni Wakazi Wa Kata Ya Matola Kijiji Cha Mtila Wamekamatwa Na Wananchi Wa Kijiji Cha Mfereke Na Kufikishwa Kituo Kidogo Cha Polisi Baada Ya Kuwatilia Mashaka Ya Wizi Wa Pikipiki.
Wakizungumza Na Uplands Fm Wananchi Wa Kijiji Cha Mfereke Wamesema Kuwa Wamewatilia Shaka Na Kuita Poilisi Kwa Uchunguzi Zaidi Baada Ya Kuona Wamefika Katika Eneo La Vibanda Vya Biashara Na Kuanza Kutengeneza Pikipiki Walizokuwa Wakitembelea Kwa Kubadilisha Enjine Na Kuweka Nyingine Za Ziada Walizo kuwa Wametembea Nazo.
Wamesema Kuwa Baada Ya Kuona Wanachana Makava Ya Pikipiki Hizo Na Kuanza Kuziweka Kwa Sura Nyingine Jambo Ambalo Limesababisha Kuwakamata Na Kuwaita Polisi Wa Kituo Kidogo Cha Uwemba Ili Wafanyiwe Uchunguzi Dhidi Ya Pikipiki Hizo Kwamba Huenda Ni Mali Za Wizi.
Mwenyekiti Wa Kijiji Cha Mfereke Bwana Carlos Damian Mlowe Amethibitisha Kuwakamata Vijana Wawili Waliohisiwa Kuwa Na Pikipiki Za Wizi Nakwamba Baada Ya Kuwahoji Na Kupewa Maelezo Yenye Mashaka Wamelazimika Kuwapeleka Katika Kituo Cha Polisi Cha Uwemba.
Bwana Mlowe Amesema Kuwa Vijana Hao Walipohojiwa Wamechukuwa Wapi Pikipiki Hizo Wamedai Walikwenda Kuzinunua Dar Es Salaama Ambapo Wananchi Na Viongozi Wa Kijiji Hicho Wakawatilia Shaka Baada Ya Kuona Wanabadilisha Injini Na Chest Cova Za Pikipiki Hizo.
Matukio Ya Wizi Wa Pikipiki Na Wamiliki Na Madereva Kushambuliwa Yalianza Kupotea Kwa Takribani Miezi Miwili Lakini Kwa Sasa Yameanza Kujitokeza Ambapo Jitihada Za Wamiliki Na Viongozi Wa Serikali Zinaendelea Ili Kudhibiti Matukio Ya Wizi Wa Mali Za Wananchi.