Aliye Kaa Kushoto ni Mfanyabiashara wa Vyombo Mjini Njombe Kaini Nyigu Akiwa Nje ya Duka Lake Kwa ajili ya Kufungua Duka Lililofungwa Kwa Siku ya Pili Sasa
milango ya maduka yaanza kufunguliwa mchana wa leo baada ya kesi kuahirishwa dodomaSerikali Imetakiwa Kuharakisha Upelelezi wa Kesi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Taifa Johnson Minja Ili Kukamilisha Utata wa Kesi ya Mwenyekiti Huyo Badala ya Kuendelea Kuwasubirisha Wananchi Kupata Mahitaji Yao Kutokana na Kufungwa Kwa Maduka.
Kauli Hiyo Imetolewa Leo na Baadhi ya Wafanyabiashara Mjini Njombe Baada ya Kuahirishwa Kwa Kesi ya Mwenyekiti Huyo Hadi Julai 16 Mwaka Huu Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Dodoma.
Wakizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Baadhi ya Wafanyabiashara Hao Wamesema Kuwa Kitendo Hicho Kinasababisha Kudorora Kwa Uchumi wa Nchi na Mtu Mmoja Mmoja Kutokana na Mufungwa Kwa Maduka Hayo.
Miongoni Mwa Wafanyabiashara Waliozungumzia Suala Hilo ni Pamoja na Mfanyabiashara Anayefahamika Kwa Jina la Kaini Nyigu Ambaye Amesema Kuwa Mbali na Serikali Kuendelea na Kesi ya Minja Mkoani Dodoma Lakini Inapaswa Iliangalie Kwa Umakini Suala Hilo Ili Wananchi Wasiendelee Kupata Adha.
Oraph Mhema ni Afisa Habari wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Njombe Ambaye Yuko Mkoani Dodoma Amesema Kesi
Hiyo Imeahirishwa Hadi Julai 16 Mwaka Huu Kwa Kile Kinachoelezwa Kushindwa Kukamilika Kwa Upelelezi wa Kesi Hiyo na Kutokamilika Kwa Mashahidi wa Kesi Hiyo Upande wa Jamhuri.
Aidha Amesema ni Vyema Serikali Ikifuta Kesi Hiyo Badala Ya Kuendelea Kuiendesha pasipo Mafanikio Kwa Kipindi Chote Hiki Ilihali Wananchi Wanaendelea Kukosa Huduma Kwa Kufungwa Maduka Kila Tarehe ya Kesi.
Awali Kesi Hiyo Ilipangwa Kusikilizwa Kwa Siku Tatu Mfululizo Katika Mahakama Hiyo Kuanzia Juni 8 Hadi 10 Mwaka Huu Lakini Taarifa Toka Mkoani Dodoma Zinaeleza Kuahirishwa Kutokana na Kukosekana Kwa Nyaraka Muhimu Katika Kesi Hiyo na Kufanya Kusikilizwa Kwa Siku Mbili.