ASKARI POLISI ANUSURIKA KUUAWA KWENYE MKUTANO WA CHADEMA


Viongozi wa Chadema wakimuokoa Askari Polisi Zakayo

Vurugu zinaendelea
Mtia nia wa ubunge  Chadema jimbo la Geita Rodgers Luhega  akiwa anamuokoa  askari polisi aliyekuwa akipigwa na wananchi mara baada ya kuonekana anarekodi mkutano wao kwa kujificha. Picha zote na na Valence Robert Geita Malunde1 blog
Askari  wa  jeshi la Polisi  mkoani Geita  Insepekta  Zakayo amenusurika kuuawa baada ya kupokea  kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira kali  kwenye mkutano wa  hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema uliofanyika mjini Geita  jana maeneo ya soko kuu la Geita.
 
Inaelezwa kuwa askari huyo ambaye alikuwa amevalia kiraia alifika katika mkutano huo akiwa na simu ambayo alionekana muda wote akirekodi kila kitu katika mkutano,na alikuwa akifanya hivyo kwa kificho.
 
Wakati akiendelea kurekodi mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Geita Alphonce Mawazo ,alipanda jukwaani na kumuona akiendelea kurekodi....akasema
 
"Maaskari tunawaheshimu sana ,tunajua kwamba kuna baadhi mnaagizwa na wakubwa zenu kuja kurekodi vitu ambavyo tunavizungumza ,sisi hatukatai mtu kurekodi,kama unataka kurekodi kwanini usije sehemu ya wazi unafanya kwa kificho “alisema.
 
Kuna askari ambaye tunamfahamu kavaa kiraia na helmenti nyekundu na yupo hapa anarekodi......"
 
Baada ya kusema hayo wananchi walimvamia askari huyo na kuanza kumpiga ngumi  maeneo mbalimbali ya mwili wake hali ambayo ilisababisha askari huyo kupata majeraha usoni  na mkutano kuvurukika kwa muda wa dakika 5.
 
Aidha baada ya  wananchi kumvamia Askari huyo Mawazo aliagiza walinzi wa chama  hicho maarufu kama  Red Briged kuwazuia  wananchi wasiendelee kumpiga huku akiwataka wananchi hao waache kumpiga Askari.
 
Hata hivyo wananchi hao hawakusikia ndipo Askari wanchadema walipoamua kutumia nguvu kwa kuwatawanya wananchi na kufanikiwa kumuokoa.
 
"Makanda mwacheni,msimpige makamanda, Red Briged kamuokoeni huyo “alisema mawazo ambapo askari hao walienda kumuokoa na muda mfupi gari ya jeshi la polisi ikiwa na askari  wa  kikosi cha kutuliza ghasia na kumpakiza kisha  kwenda kituoni naye kituoni wakiwa na makamanda wa Chadema",alisema
 
Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Peter Kakamba alikili kutokea kwa tukio hilo na  kwamba uchunguzi bado unaendelea wa kubaini waliofanya tukio hilo.
 
“Ni kweli kuna Askari wetu amepigwa,lakini tunaendelea na uchunguzi wa kuwatafuta watu waliomshambulia askari huyo na nitatolea ufafunizi kesho saaa 4:00 asubuhi".
 
Hata hivyo baada ya vurugu hizo kuisha mkutano huo  uliolenga kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura linalotarajia kuanza Juni 9 mwaka huu mkoani humo uliendelea ,ambapo Mawazo  alimlalamikia  Mkurugenzi wa Halmasahuri ya mji Margareth Nakainga kwa kuweka vituo vichache vya kujiandikisha na kudai hali hiyo ni njama za CCM .
 
“Inashangaza mji wa Katoro ulivyo mkubwa na watu wengi, lakini wameweka kituo kimoja cha kujiandikisha,hii inaonyesha  wengi hawatajiandikisha kwani wengi watatembea umbali mrefu zaidi ya km 8,na walivyowajanja maeneo mengi ambayo chadema imeshinda  uchaguzi wa serikali za mitaa ndiko wamepeleka vituo vichache”alisema Mawazo.
 
Pia alitoa angalizo kwa tume ya uaNdikishaji kuwa makini kutatua tatizo hilo mapema  ili yasitokea machafuko kwani wananchi hawatakubali  kuona wenzao wanandikishwa na wengine kuachwa na kwamba  utaungana nao  kufanya maandamano makubwa yasiyo kuwa na kikomo ili kupinga hujuma hizo.
 
Aidha katioka mkutano huo baadhi ya watia nia wa kiti cha ubunge na udiwani jimbo la Geita mjini  walijitokeza  rasmi na kutanga za nia yao ya kugombea nafasi hizo  katika jimbo  hilo ambapo nafasi ya ubunge walijitokeza  saba na   udiwani zaidi ya 10 na kuwaomba wananchi kuwaunga mkono ili kulikomboa jimbo hilo.
 
Na Valence Robert-Malunde1 blog Geita