ZOEZI la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura Kwa mfumo wa
Biometric voters regstetion ( BVR) linaloendelea mkoani Njombe katika
mji mjimdogo wa Makambako jana lilitakiwa kufukia mwisho huku watu
zaidi wa 38,000 wanatarajiwa kuandikishwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Njombe msimamizi wa zoezi
hilo katika kata ya Mjimwema, Hamza Mandwanga, alisema kuwa hali ya
uandikishaji inaendelea vizuri na kuwa anaomba kama kutaweza kuongezwa
siku moja ili kufikia lengo la kuandikishwa wakazi hao.
Alisema kuwa mashinehizo zinauwezo wa kuandikisha watu zaidi wa 100,
ambapo watu wanapungua kadri siku zinaongezeka kwa kuwa siku za kwanza
watu waliandishwa wengi.
Alisema kuwa katika vitu alivyo tembelea waliohamasika kujiandikisha
ni vijana zaidi kuliko lika lingini kutokana na hamasa iliyo tolewa.
"Katika zoezi hili watu walio jitokeza kujiandikisha wengi wao
walikuwa ni vijana wa miaka ya 1980 na kuendelea na kama ninepewa
nafasi ya kutoa ushauri ningependekeza kuongezeke siku moja ili wale
watakao baki leo katika foleni waandikishwe siku ninafo fuata,"
alisema Mandwanga.
Kwa upande wake mwenyekiwa wa mtaa wa mtaa wa Mlando, John Mbata
alisema kuwa katika mtaa huo watu wamejitokeza kwa wingi na kuwa watu
katika mtaa wake wamejiandikisha wote na kuwa wameanza kujitokeza watu
kutoka mtaa wa jirani.
Alisema kuwa katika mtaa wake watu wengi wamejiandikisha na kuwa
anatoa wito kwa ambako zoezi linaenda na kuwa mashine ziwe mbili ili
zoezi hilo kuwa na ufanisi zaidi.
"Katika mitaa ambako zoezi linaelekea tume wajitahidi kuweka mashine
zaidi ya moja kwa mitaa mikubwa na mitaa midogo kutokana na idadi ya
watu mashine moja ili kuhakikisha zoezi linaenda bila matatizo,"
aliongeza Mbata.
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya mji makambako, Chesco Mfikwa,
alisema kuwa zoezi hilo limeenda vizuri na kuwa wamefanikiwa kwa siku
ya juzi wameandishishwa watu zaidi ya 32,000.
Alisema kuwa kufikia jana jione wangeweza kuandikisha watu 6,000 kwa
siku hiyo na kufikia idadi ya watu 38,000, ambapo wameweza kufikia
zaidi ya asilimia 80.
Alisema kuwa katika zoezi hilo siku za kwanza walikuwa watu
wakiandikishwa wachache na kuongezeka wa kwa siku hasa vijana na
kufikia hadi watu 6500 kwa siku.
Alisema kuwa zoezi linakoendelea watu watakao kuwa wanahudumu
kuandikisha wapatiwe elimu ya kutosha ili waweze kukabiliana na
changamoto zinazo weza kujitokeza hasa namna ya kutumia mashine za
BVR.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)