Wachezaji wa Jambo Leo mpira wa miguu (wenye jezi rangi nyekundu) wakitoka uwanjani mara baada ya kufungwa goli la 3 na kususia mchezo huo kwa madai uwanja umeharibika kwa kujaa maji. Mchezo huo ulivunjika katika dakika 69.Wachezaji wa timu ya NSSF mpira wa miguu wakitoka uwanjani huku wakipongezana mara baada ya mwamuzi kumaliza pambano lao na timu ya Jambo Leo. NSSF walipewa ushindi wa magoli 3-0. Baada ya Timu ya Jambo Leo kukimbia uwanjani baada ya kufungwa goli la 3 katika dakika 69 ikisingizia uwanja mbaya.Wachezaji wa timu ya NSSF mpira wa miguu wakitoka uwanjani mara baada ya mwamuzi kumaliza pambano lao na Jambo Leo na kupewa ushindi wa magoli 3-0. Timu ya Jambo Leo ilikimbia uwanjani baada ya kufungwa goli la 3 katika dakika 69 ikisingigia uwanja mbaya.Baadhi ya viongozi na wachezaji wa akiba wa Timu ya Uhuru Media wakifuatilia pambano lao na Sahara Media.Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru FM, Angel Akilimali (kulia) akishirikishana jambo na mmoja wa viongozi wa timu yake uwanjali. Katika mchezo huo Uhuru ilishinda bao 2-1.Mshike mshike Mpira wa Pete, wachezaji wa New Habari (rangi njano) pamoja na wachezaji wa timu ya Business Times wakichuana, B/Times ilishinda mchezo huo kwa magoli 46-2Mchezaji wa Mpira wa Pete wa Business Time (mwenye mpira) akijiandaa kufunga katika goli la New Habari, B/Times ilishinda mchezo huo kwa magoli 46-2.Baadhi ya maofisa na wafanyakazi wa Shirika la NSSF wanaoendelea kutoa huduma mbalimbali za NSSF kwa wateja wanaofika viwanja vya TTC Changombe kufuatilia mashindano ya NSSF Media Cup wakiwa katika picha ya kumbukumbu kwenye banda la huduma.Kikosi cha Uhuru FM (wenye njano na bluu) kikipiga picha ya kumbukumbu pamoja na mwamuzi wa mchezo na mchezaji mmoja wa timu pinzani. Katika mchezo huo Uhuru ilishinda bao 2-1.Kiosi cha Sahara Media kikipiga picha ya pamoja kabla ya kupambana na Uhuru Media. Katika mchezo huo Uhuru ilishinda bao 2-1.Baadhi ya wachezaji wa Jambo Leo wakiwa wamesimama nje ya uwanja baada ya kuweka mpira kwapani mara baada ya kufungwa goli la 3 katika dakika 69. Mwamuzi wa mpambano huo aliamua kumpa ushindi NSSF baada ya Jambo Leo kutoka uwanjani.Baadhi ya wachezaji wa akiba wa timu ya NSSF wakifuatilia tukio la kusimama kwa pambano kati yao na Jambo Leo dakika ya 69. NSSF hadi mpira unasimama ilikuwa ikiongoza kwa goli 3-0.
Mpira wa Pete, New Habari Waogelea Magoli 46-2
MASHINDANO ya NSSF Media Cup yameendelea kupamba moto ambapo timu ya mpira wa miguu ya NSSF imeichalaza bila huruma timu ya Jambo Leo kwa magoli 3 kwa mtungi. Mchezo huo mkali ambao uliwafanya wachezaji wa timu ya Jambo Leo kukimbia uwanjani kutokana na mvua ya magoli mfululizo ulivunjika dakika ya 69.
Mwamuzi wa mpambano huo alilazimika kumaliza mchezo baada ya kuwasubiri wachezaji wa Jambo Leo kurudi uwanjani kwa dakika 15 bila ya mafanikio kisha kuamua kumaliza pambano na kutoa ushindi kwa timu ya NSSF. Hadi pambano hilo linasimama katika dakika ya 69 NSSF ilikuwa ikiongoza kwa magoli 3 kwa mtungi.
Wachezaji wa Jambo Leo walitoka uwanjani kwa kudai hawawezi kumalizia mchezo huo kutokana na hali ya uwanja ambapo ulikuwa umejaa madimbwi ya maji kwa baadhi ya maeneo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.
Jambo Leo waliomba pambano hilo lisimamishwe na kuendelea kesho au siku nyingine ambapo uwanja ulikuwa katika hali nzuri tofauti na ilivyokuwa.
Hata hivyo Kamisaa wa Mchezo huo, Majuto Omary alisema mpambano huo hauwezi kurudiwa maana kanuni za mashindano haziruhusu na kuongeza kuwa kama Jambo Leo waliona uwanja ni mbovu wangeligoma tangu awali na sio kusubiri mchezo uchezwe hadi dakika ya 69.
"...Kanuni za mashindano haya haziruhusu wanachotaka Jambo Leo, kwanini wakimbie uwanjani baada ya kufungwa magoli matatu...mbona hawakugoma tangu mchezo haujachezwa hii ni janja yao wameona wamefungwa tena magoli mengi ndio wakimbie uwanja hii haikubaliki, ushindi utaenda kwa aliyeshinda na pambano halirudiwi," alisema Omary.
Mvua ya magoli nyingine katika mashindano hayo iliwakumba timu ya Mpira wa Pete wasichana ya New Habari ambapo ilichalazwa magoli 46 kwa mawili na timu ya Business Times wasichana katika mchezo wao uliofanyika TTC Chang'ombe. Katika mchezo huo Business Timu walionekana kuutawala mchezo kwa muda wote na kuwapeleka puta akinadada wa New Habari kabla ya kuogelea mvua hiyo ya magoli.
Katika mchezo mwingine wa mpira wa miguu, Timu ya Uhuru Media iliichapa Sahara Media kwa magoli 2-1. Timu ya Sahara ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli ambapo walipachika bao la kwanza katika dakika 26 kupitia kwa mchezaji wao Deodatus Nkwabi alilofunga kwa kichwa. Uhuru walikuja juu dakika 46 ambapo mchezaji wao Mussa Gadi alifunga goli kwa mpira wa adhabu na kusawazisha mchezo. Mchezaji wa Uhuru Media, Ayub Malale alicheka na nyavu za Sahara Media katika dakika 87 baada ya kuunganisha crosi na kufanikiwa kufunga bao la pili. Hadi mwisho wa mchezo huo Uhuru 2 na Sahara 1.
Mashindano ya NSSF Media cup yanaendelea katika viwanja vya TCC Chang’ombe na Bandari Jijini Dar es Salaam, yakihusisha mpira wa miguu na mpira wa Pete ambapo vyombo mbalimbali vya Habari vinashiriki michezo hiyo. Mashindano hayo yanaambatana na wiki ya Huduma Kwa wateja ya NSSF ambapo wateja watapata fursa ya kupata elimu kuhusu huduma za NSSF.
Kama wewe ni Mkazi wa Dar es Salaam Tafadhali tembelea banda la NSSF katika viwanja vya TCC Chang’ombe kuanzia Tarehe 20/03/2015 hadi Tarehe 29/03/2015 saa 03:00 asubuhi hadi 11:00 jioni.
Mwanachama ataweza kupata taarifa ya michango yake, Kujiandikisha Kwa Wanachama wapya na vile vile watapata elimu kuhusu huduma mbalimbali za NSSF.