WANAHABARI WAHIMIZWA KUWASILISHA MASUALA YAHUSUYO WATOTO YATIMA NA WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU


SAM_0796
Vyombo vya habari nchini vimehimizwa kuwasilisha masuala yanayowahusu watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu. Akizungumza na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali jijini Arusha katika warsha juu ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoendeshwa na shirika liliso la kiserikali la The Foundation For Tomorrow (TFFT).
 
Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania wa shirika hilo, Bwa. Kennedy Oulu alisema tatizo la watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu nchini Tanzania ni gumu, hivyo vyombo vya habari havina budi kuifahamisha jamii kuhusu hili suala na matatizo yanayowakabili watoto yatima na waishio katika mazingira magumu ili jamii na wadau mbalimbali waweze kushiriki vema katika kukabiliana na tatizo hili.
 
“Kwa sasa, inakadiriwa kuwa kuna watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu wapatao 1,800,000 hapa Tanzania pekee, huku 1,300,000 kati yao wakiwa wametokana na athari za ugonjwa wa UKIMWI. Mgawanyo wa kifamilia na muundo wa kimsaada kijamii ni moja ya vinavyochangia tatizo hili. 

Vinapoongezwa katika umaskini unaojidhihirisha katika: ukosefu wa upatikanaji wa huduma za elimu ikiwemo elimu ya awali, ukosefu wa upatikanaji wa huduma za afya na uzalishaji kama afya ya uzazi, ukosefu wa stadi za maisha zinazoakisiwa katika mitaala ya shule zenye uwezo unaotakiwa na ubunifu ili kujenga uwezo wa watoto, si kwa yatima na waishio katika magumu pekee”. Alisema Kennedy na kuongeza.
 
“Ni muhimu kutambua kuwa kumekuwa na hatua na mafanikio yaliyofikiwa na wadau mbalimbali ikiwemo serikali katika kuwezesha upatikanaji, kuzijengea uwezo familia za watoto hawa na kubadili mitazamo ya jamii dhidi ya watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu, hii inajenga msingi wa mwitikio endelevu.