Showing posts with label Arusha. Show all posts
Showing posts with label Arusha. Show all posts

CHADEMA Jimbo la Moshi Mjini Yatangaza Wagombea.Wake.

Mkutano wa Hadhara wa Kampeni wa Utamburisho wa wagombea wa Udiwani katika jimbo la Moshi mjini.

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Korongoni ,manispaa ya Moshi,Ally Mwamba akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Korongoni (hawapo pichani).

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Rau ,manispaa ya Moshi,Peter Kimaro akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Rau (hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Ng'ambo ,manispaa ya Moshi,Genesis Kiwelu akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Ng'ambo (hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Miembeni,manispaa ya Moshi,Mbonea Mshana akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Miembeni (hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Msaranga ,manispaa ya Moshi,Anna Mushi akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Msaranga.(hawapo pichani).

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Bomambuzi ,manispaa ya Moshi,Ludos Tarimo  akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Bomambuzi(hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Majengo,manispaa ya Moshi,Peter Minja akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Majengo (hawapo pichani)
Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Kilimanjaro ,manispaa ya Moshi,Afrikan Mlay  akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi kata ya Kilimanjaro (hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Korongoni ,manispaa ya Moshi,Charles Mkome Mkalakala akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Pasua (hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Kaloleni ,manispaa ya Moshi,Francis Shio akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Kaloleni (hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Kiusa ,manispaa ya Moshi,Stephen Ngasa akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Kiusa .
Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Kaloleni ,Manispaa ya Moshi,Reward Shelukindo akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Kaloleni  (hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Shirimatunda,manispaa ya Moshi,Makupa Jonathan akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Shirimatunda. (hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Mawenzi ,manispaa ya Moshi,Hawa Mushi  akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Mawenzi (hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Mji Mpya ,manispaa ya Moshi,Abuu Shayo akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Mji Mpya .

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Nganga mfumuni ,manispaa ya Moshi,Anthony Lyimo  akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Mfumuni(hawapo pichani

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Soweto ,manispaa ya Moshi,Collins Tamimu akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Soweto.
Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Njoro ,manispaa ya Moshi,Jomba Koi akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Soweto.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Gola kuondoa watoto wa Mitaani Arusha

Afisa ustawi wa jamii na Maendeleo ya jamii jijini Arusha  Mwantumu Dossiakitembelea mradi wa shamba la mahindi unaoendeshwa na taasisi ya Gola
Foundation jana katika kituo cha Kufikia watoto wa mitaani,katikati ni
Mkurugenzi wa shirika hilo  Elisha Maghembe
Mkurugenzi wa shirika lisilokua la kiserikali la Gola Foundation ,Elisha Maghembe amesema kuwa wameanza zoezi la  kuwaondoa watoto wa mitaani walioko  jijini Arusha na kuwafikisha kwenye vituo maalumu vya malezi lengo ikiwa ni kuwarudisha makwao pamoja na kuwapatia fursa ya elimu waliyoikosa kwa muda mrefu.

Elisha alisema kuwa zoezi hilo limeanza mapema mwaka huu ambapo mpaka sasa wamewakusanya watoto 25 na kuwapeleka katika kituo chao cha malezi kilichopo wilaya ya Arumeru ambapo watoto watano walitambuliwa na kuchukuliwa na wazazi wao.

Amesema kuwa watoto wa mitaani wanapokaa mtaani kwa muda mrefu hujitumbukiza katika majanga ya matumizi ya madawa ya kulevya na kufanya vitendo visivyofaa hivyo ameitaka jamii ishirikiane kutatua tatizo hili ambalo ni janga kwa taifa.

“Tunapofika mtaani kuwaondoa watoto hawa wa mtaani tunakutana na changamoto nyingi ikiwemo kukosa ushirikiano na watoto wenyewe na pia wengine wanatumkishwa na ajira katika umri mdogo na baadhi ya watu hivyo kufanya zoezi hilo kuwa gumu” Alisha Elisha

Afisa ustawi wa jamii na Maendeleo ya jamii jijini Arusha,  Mwantumu Dossi alifika katika kituo cha kufikia cha malezi ya watoto wa mtaani kinachomilikiwa na Gola Foundation amesema kuwa Halmashauri ya jiji itaangalia namna ya kushirikiana kutatua changamoto za watoto wa mitaani.

“Tatizo la watoto wa mitaani ni tatizo sugu nimefika apa kujionea na kama Jiji kuna mkakati Mahususi wa kuwaondoa watoto wa mitaani utakaoanza 2015-2016” alisema Mwantumu 

Mwenyekiti wa Baraza la watoto wilaya ya Arusha Hassan Omari alisema kuwa juhudi za kuwaondoa watoto wa mitaani katika mazingira magumu na hatarishi zinapaswa kuungwa mkono na kila mtu pamoja na serikali kwani watoto ni taifa linalotegemewa kesho. 

WANAHABARI WAHIMIZWA KUWASILISHA MASUALA YAHUSUYO WATOTO YATIMA NA WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

SAM_0796
Vyombo vya habari nchini vimehimizwa kuwasilisha masuala yanayowahusu watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu. Akizungumza na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali jijini Arusha katika warsha juu ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoendeshwa na shirika liliso la kiserikali la The Foundation For Tomorrow (TFFT).
 
Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania wa shirika hilo, Bwa. Kennedy Oulu alisema tatizo la watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu nchini Tanzania ni gumu, hivyo vyombo vya habari havina budi kuifahamisha jamii kuhusu hili suala na matatizo yanayowakabili watoto yatima na waishio katika mazingira magumu ili jamii na wadau mbalimbali waweze kushiriki vema katika kukabiliana na tatizo hili.
 
“Kwa sasa, inakadiriwa kuwa kuna watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu wapatao 1,800,000 hapa Tanzania pekee, huku 1,300,000 kati yao wakiwa wametokana na athari za ugonjwa wa UKIMWI. Mgawanyo wa kifamilia na muundo wa kimsaada kijamii ni moja ya vinavyochangia tatizo hili. 

Vinapoongezwa katika umaskini unaojidhihirisha katika: ukosefu wa upatikanaji wa huduma za elimu ikiwemo elimu ya awali, ukosefu wa upatikanaji wa huduma za afya na uzalishaji kama afya ya uzazi, ukosefu wa stadi za maisha zinazoakisiwa katika mitaala ya shule zenye uwezo unaotakiwa na ubunifu ili kujenga uwezo wa watoto, si kwa yatima na waishio katika magumu pekee”. Alisema Kennedy na kuongeza.
 
“Ni muhimu kutambua kuwa kumekuwa na hatua na mafanikio yaliyofikiwa na wadau mbalimbali ikiwemo serikali katika kuwezesha upatikanaji, kuzijengea uwezo familia za watoto hawa na kubadili mitazamo ya jamii dhidi ya watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu, hii inajenga msingi wa mwitikio endelevu.

Kategori

Kategori