Breaking News: Baraza lafanyiwa mabadiliko soma hapa..........

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko la baraza la mawaziri kwa kuwateua mawaziri wapya wanane na manaibu waziri watano.
Akitangaza Mabadiliko hayo Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema wapya waliongia katika Baraza hilo ni Anne Kilango Malecela na Charles Mwijage.
Mabadiliko hayo yako kama ifuatavyo:-
George Simbachawene aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameteuliwa kuwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini.
Mary Nagu aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu).
Eng. Christopher Chiza aliyekuwa Waziri Kilimo, Chakula na Ushirika ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji).
Dkt Harrison Mwakyembe aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi ameteuliwa kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Wiliam Lukuvi aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Stephen Wasira aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais , (Mahusiano na Uratibu) ameteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika.
Samuel Sitta aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ameteuliwa kuwa Waziri wa Uchukuzi.
Jenister Mhagama aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge)
Stephen Maselle aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini ameteuliwa kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano)
Angela Kairuki aliyekuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria ameteuliwa kuwa Naibu Waziri Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Ummy Mwalimu aliyekuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria.
Anne Kilango Malecela mbunge wa Same Mashariki ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Je una maoni gani kuhusu mabadiliko haya?
Charles Mwijage Mbunge wa Muleba Kaskazini ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini