NDUGU ABDULRAHMAN KINANA SHAMBANI KIJIJI CHA KWEMNYEFU

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kulima na kupanda mahindi katika shamba kijijini Kwemnyefu Kata ya Mpapayu wilayani Mheza mkoani Tanga pamoja na wananchi wakati alipotembelea shamba hilo na kukagua shughuli za kilimo cha mkono, Katika shughuli hiyo katibu mkuu huyo ameshirikiana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, Katibu Mkuu huyo kesho anaelekea wilayani Pangani baada ya kumaliza ziara yake wilayani Muheza leo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MUHEZA-TANGA)3Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi naye akishiriki pamoja na vijana kulima shambani katika kijiji cha Kwemnyefu wilayani Muheza leo.4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea na kazi shambani pamoja na vijana wa kijiji cha Kwemnyefu kata ya Mpapayu5Vijana nao wakiendelea na kazi ya kilimo shambani6Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi pamoja na vijana wakirejea huku majembe yao yakiwa begani baada ya kumaliza kazi ya kupanda mahindi shambani7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi pamoja na vijana wakirejeawakirejea huku majembe yao yakiwa beganibaada ya kumaliza kazi ya kupanda mahindi shambani8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Kilulu wilayani Muheza.9Jengo la Kituo cha habari za kilimo lililojengwa na serikali katika kata ya Songa wilayani Muheza ,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amelitembelea na kukagua ujenzi wa jengo hili. 13Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa I. M. Matovu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza wakati alipotembelea kituo cha Afya Muheza na kukagua ujenzi wa miundo mbinu kadhaa kabla kituo hicho hakijapandishwa hadhi na kuwa Hospitali ya Mbaramo Ubwari wilaya ya Muheza.14Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Jitegemee mjini Muheza.16Peter John Jambele Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ili kuongea na wananchi wa Muheza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Jitegemee mjini Muheza Tanga.17Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongeza na wananchi wa Muheza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Jitegemee mkoani Tanga.