Mtoto wa kizazi cha 'msaada' azaliwa

Womb Transplant baby
Mwanamke mmoja nchini Sweden amejifungua mtoto kutokana na kizazi alichowekewa kupitia upasuaji.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 36 alizaliwa bila kizazi kabla ya kuwekewa kizazi cha mwanamke aliyekuwa katika miaka yake ya sitini.
Jarida la afya la Uingereza ,the Lancet linasema kuwa mtoto huyo alizaliwa kabla ya mda wake kufika mnamo mwezi Septemba akiwa na uziti wa kilo1.8.
Babaake amesema mwanawe ni wa kushangaza.
Matibabu ya ugonjwa wa saratani pamoja na kasoro za mazazi ndio sababu kuu zinazosababisha wanawake kuwa na kizazi kibaya.
Iwapo wanataka kujipatia mtoto basi hulazimika kutumia mwanamke mwengine anayebeba mimba hiyo kwa niaba yake.
Ijapokuwa wazazi wa mtoto huyo hawajatambuliwa ,inaaminika kuwa mwanamke huyo alikuwa na mbegu zilizokuwa zikifanya kazi.
Kulingana na baba ya mtoto huyo ,mwanawe hana tofauti yoyote na watoto wengine.