Na.Mwashungi Tahir Maelezo.
Iko haja kubwa jamii kuwaheshimu wazee kwani bila ya wao kutulea kwa kutupa malezi mazuri kwa kutusomesha tusingelikuwa leo tuko hapa.
Hivyo iko haja kuwatunza , kuwalea na kuwathamini kwa malezi mema yao waliyotupa .
Hayo ameyasema mkuu wa Mkoa mjini magharibi Abdullah Mwinyi Khamis wakati alipokuwa akizungumza na wazee huko Dole wilaya ya magharibi katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani .
Amesema wazee wametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii katika ujana wao katika kushiriki mambo mbali mbali ya kiuchumi kiutamaduni na vile vile kijamii katika serikali.
Hivyo tunahitaji kuwalea wazee kwa kuwatunza kwa kuwapa huduma zikiwemo malazi kivazi pia ikiwemo huduma ya kuwapatia chakula waweze kuwa na siha nzuri katika maisha yao.
“Serikali inatoa mchango mkubwa katika kuwaenzi wazee hao mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu mzee Karume aliwashughulikia kwakuwajengea nyumba za kuishi wazee hao pamoja na huduma nyengine zote za jamii” alisema Abdullah Mwinyi
Abdullah Mwinyi ametoa wito kwa jamii iachane kuwatelekeza Wazee na kutoa msisitizo kwa kuwahifadhi na kuwapa huduma nzuri kama ilivyo kwa kawaida kwa binaadamu.
Nae Katibu Mkuu wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii , Vijana , Wanawake na Watoto Asha Ali Abdullah amesema serikali imepitisha sera ya hifadhi jamii ya kulinda na kuwahifadhi wazee kwa vizuri.
Siku hii ni siku muhimu inasherehekewa Duniani kote kila ifikapo tarehe 1-10-2014 ambapo ujumbe wa mwaka huu (WAZEE WASIACHWE NYUMA TUJENGE JAMII SHIRIKISHI).
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali akiwemo Katibu mkuu Mufti shekh Soraga na M kuu wa Wilaya magharibi Ayoub Moh'd Mahmoud