Hatimaye
kundi la”Wakali sisi” lenye makazi yake Kiwalani jijini Dar es Salaam,
ambalo lilikuwa miongongoni mwa makundi matano yaliyoingia fainali za
shindano la kucheza muziki maarufu kama Dance 100% linaloratibiwa na
Kituo cha East Africa Television ltd na kudhaminiwa na kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom Tanzania, limeibuka mshindi katika shindano hilo
lililokuwa la kukata kwa shoka kwa ushindani mkali katika Viwanja vya
Don Bosco, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mratibu
wa shindano hilo Happy Shame alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa,
fainali za shindano hilo ambalo safari yake ilianza Julai 19, mwaka huu
kuanzia hatua ya kusaka washiriki hadi mchujo lilishirikisha makundi
matano.
Shame
alisema, shindano la mwaka huu lilikuwa gumu na lenye kuleta msisimko
wa aina yake zaidi kuliko miaka miwili iliyopita baada ya mambo
mbalimbali kuboreshwa na zaidi kiasi cha vijana kuwa wabunifu na kuona
ni fursa kwao sio tu kupata fedha, pia kuendeleza vipaji vyao na
kujinasua kiajira.
“Ushindani
umekuwa mkubwa sana katika shindano la mwaka huu ikilinganishwa na
miaka mingine kutokana na sababu mbalimbali. Shindano pia limeanza
kupata mashabiki, tunashukuru sana sapoti ya wadhamini wetu Vodacom
Tanzania,” alisema.
Naye
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu,alieleza kwa
niaba ya kampuni aliridhishwa kabisa na matokeo na aliwapa pongezi
kundi la wakali sisi kwa kuipuka na ushindi huo.
Nkurlu
alisema kuwa, kundi hilo lilistahili ushindi kwasababu lilikuwa makini
na kufurahia kwa kile walichokuwa wanakifanya kwa moyo mkunjufu na
kujitambua kana kwamba wapo kazini.
Alisema
kampuni ya Vodacom inajivunia na kujisikia fahari kwa kudhamini
shindano hilo kwa njia hiyo ya udhamini wakitambua umuhimu wa vijana
kujiajiri kupitia vipaji vyao na kuongeza kuwa, kwa kipindi chote cha
mchakato wa shindano hilo, amejifunza mengi kutoka kwa vijana hao
walioshiriki katika shindano hilo kuwa ubunifu ni kitu muhimu sana.
“Vijana
wameonyesha uwezo mkubwa kuanzia hatua ya mchujo hadi sasa kiasi cha
kuwapa majaji wakati mgumu. Tunaamini hata baada ya fainali hizi, vijana
hawa watajiendeleza zaidi kimuziki,” alisema Nkurlu.
Makundi
matatu yaliyofanikiwa kujinyakulia zawadi mbalimbali katika hatua ya
fainali hiyo na vijana walikuwa wakionesha vipaji na umahiri mkubwa wa
kucheza staili mbalimbali za muziki ambayo ni Wakali sisi walioibuka
kidedea na kujinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5 huku kila mshiriki
katika katika kundi hilo akipatiwa simu aina ya Vodafone ikiwa na muda
wa maongezi wa sh. 100,000.
Mshindi
wa pili ni kundi la The W.T. na kuondoka na kitita cha shilingi Milioni
1 na laki 5 na mshindi wa tatu ni kundi la Wazawa Crew na kujinyakulia
shilingi laki 5.
Nkurlu
aliyapongeza makundi yote hata ambayo hayakufanikiwa kushinda na
kuyatakia kila la heri na yatipange upya kwa mwakani kwani asiye kubali
kushindwa si mshindani aliongeza kuwa, kwa vile vijana hao wamejiweka
katika mazingira ya kutumia vipaji vyao kujipatia ajira, Kampuni ya
Vodacom-Tanzania inaona fahari kudhamini shindano hilo wakisaidia juhudi
za serikali kupambana na tatizo la ajira.
“Takwimu
zinaonesha kuwa kila mwaka vijana zaidi ya 800,000 wanaingia katika
soko
la kusaka ajira ndio maana, Vodacom Tanzania kwa kulitambua hilo,
tumekuwa mstari wa mbele kusaidiana na serikali na wadau wengine
kuwajengea vijana msingi,” alisema Nkurlu.
Kikundi cha The WT cha jijini Dar es Salaam
kilichoshinda nafasi ya pili katika fainali ya shindano la Dance 100% 2014
likionesha umahiri wao wa kudansi katika fainali hiyo iliyofanyika mwishoni mwa
wiki katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam.Ambapo kundi
la”WAKALI SISI”toka kiwalani jijini liliibuka na ushindi huo na kujinyakulia
kitita cha shilingi Milioni 5 toka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo Vodacom
Tanzania.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia)
akitaniana na kiongozi wa kundi la”Wakali sisi”la kiwalani jijini Dar es Salaam,Baraka
Kambona(kushoto)alipokuwa akikabidhi hundi yenye thamani ya Tsh Milioni 5 kwa
kundi hilo kama wadhamini wakuu wa shindano la Dance 100% kundi hilo liliibuka
washindi katika fainali ya shindano hilo
lililofanyika mwishoni mwa wiki Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Washindi wa shindano la Dance 100% 2014 kundi la
wakali sisi wakiwa kwenye picha ya pamoja na majaji wa shindano hilo na Ofisa
matukio wa Basata Kurwijira Magesa (kushoto)pamoja
na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(wapili toka kulia)
mara baada ya kutangazwa washindi wa shindano hilo na kujinyakulia kombe pamoja
na kitita cha shilingi milioni 5 toka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo Vodacom
Tanzania.
Washiriki
wa shindano la dance 100% wa kundi la ”The Winners Crew” la jijini Dar es
Salaam,wakionesha umahiri wao wa kudansi wakati wa mchuano wa fainali wa
shindano hilo lililoandaliwa na EATV lililofanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini
Dar es Salaam,ambapo kundi la”WAKALI SISI” liliibuka washindi na kunyakua kitita
cha shilingi Milioni 5 toka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo Vodacom
Tanzania.
Meneja mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya
Kinondoni, Edward Byampanju(kushoto)na Meneja uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina
Nkurlu(katikati)wakijadiliana jambo wakati wa fainali ya shindano la Dance 100%
2014.ambapo kundi la”Wakali sisi”liliibuka washindi na kukabidhiwa kitita cha shilingi milioni 5 na wadhamini
wakuu wa shindano hilo Vodacom Tanzania,watatu toka kushoto ni Afisa Matukio wa Basata, Kurwijira Maregesi.
Kundi la”Wakali sisi”ambao ni mabingwa wa
shindano la Dance 100% 2014,wakionesha umahiri wao wa kucheza wakati wa fainali
ya shindano hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Don Bosco
Oysterbay jijini Dar es Salaam na kuweza kujinyakulia kitita cha Tsh Milioni 5 toka
kwa mdhamini mkuu wa shindano hilo Vodacom Tanzania.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliofurika
katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam kushuhudia mchuano
mkali wa fainali ya Dance 100% ambapo kundi la Wakali sisi liliibuka na ushindi
na kuweza kuondoka na kitita cha shilingi Milioni 5 toka kwa mdhamini mkuu wa
shindano hilo Vodacom Tanzania.