
Mshambuliaji
wa Yanga, Didier Kavumbagu (kushoto) akiruka kuwania mpira na kipa wa
Ashanti United, Daudi Mwasongwe, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya
Tanzania Bara uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar
es Salaam. Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi wa mabao
2-1,yaliyofungwa na Didier Kavumbagu katika dakika ya 51 na la pili
likifungwana David Luhende katika dakika ya 79.
Bao la Ashanti lilifungwa na Bright Obina katika dakika ya 61.
Katika
michezo mingine, huko katika uwanja wa Chamazi Azam 1-Mtibwa Sugar 0,
katika uwanja wa Mkwakwani Tanga Coastal Union 1- JKT Oljopro 1, Uwanja
wa Kaitaba Kagera Sugar 0-Mbeya City 1 mpira bado unaendelea.
Mshambuliaji
wa Yanga, Mrisho Ngassa (katikati) akijaribu kuwatoka mabeki wa
Ashanti, Abuu Mtiro (kushoto) na Iddi Seleman (kulia).
Wachezaji wa Yanga wakimpongeza mwenzao, David Luhende baada ya kufunga bao la pili.
Hussein Javu, akiruka kujaribu kumchambua kipa wa Ashanti.
Mohamed Fakhi na Hussein Javu, wakiwania mpira.
Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm, akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.
Kocha
akizungumza na wachezaji wake baada ya mchezo kumalizika. Simba
watashuka dimbani katika uwanja wa Taifa kesho kukipiga na Rhyno.
Na Matukio na Vijana