Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Athuman Livigha
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Athuman Livigha, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi nyumbani kwake, jijini Dar es Salaam.
Taarifa za kifo hicho zilithibitishwa na Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala, alipozungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana.
Profesa Mukandala alisema Profesa Livigha alikutwa na masaibu hayo akiwa nyumbani kwake Bunju, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia jana na kwamba, mwili wake umechukuliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.
“Ni kweli, na mimi hizo habari tumezipata na watu wote wamekwenda nyumbani kwake. Mwili umechukuliwa na polisi, tunasubiri taarifa kutoka polisi,” alisema Profesa Mukandala bila kufafanua zaidi.
Aliongeza: “Mimi nilikuwa mjini, wenzangu wamekwenda nyumbani kwake Bunju. Tumesikitishwa sana kwa kupotelewa na mwalimu wetu mwingine katika mazingira kama hayo.”
Profesa mwingine wa UDSM, Jwani Kwaikusa, aliuawa Julai, 2010 kwa kupigwa risasi na watu waliodaiwa kuwa ni majambazi
Na matukio na wanavyuo