Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias
(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya
maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB,
Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo.

Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed
Ramadhan (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited,
Marion Elias.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias
(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya
maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam.
Katikati ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB,
Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo na kulia ni Meneja Bidhaa za
Azam, Abubakar Suleiman.
KAMPUNI
ya Insights Productions Limited kwa udhamini wa Kampuni ya Azam
Tanzania imeandaa maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika
jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa uandaaji na
utayarishaji wa keki.
Maonesho
hayo yatajulikana kama 'Azam World of Cakes Exhibition'.
Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa
Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias alisema maonesho
hayo yanatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali binafsi, makampuni na
taasisi waandaaji wa keki nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya
kubadilishana uzoefu na kujifunza ubunifu zaidi wa shughuli hizo.
Bi.
Elias alisema dhumuni la maonesho hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika
Desemba 6, 2014 jijini Dar es Salaam ni pamoja na kusherehekea taaluma
ya uokaji keki kwa kuonesha ubunifu na utaalam wa utengenezaji na
upambaji wa keki bidhaa inayopendwa na watu wengi na kutumika katika
shughuli anuai za kijamii.
Alisema
washiriki wa tamasha hilo mbali na kushindanisha na kuonesha bidhaa zao
za keki pia wanatarajia kupata semina ya mafunzo juu ya utengenezaji
bora wa keki ikiwa na lengo la kuboresha zaidi taaluma zao.
Alisema washiriki hao pia watafanya maonesho ya utayarishaji wa vyombo
vya kutengenezea keki, utayarishaji wa unga wa ngano kwa ajili ya
kupikia keki, kutambua unga bora wa keki, uchanganyaji wa unga na viungo
vingine kwa ajili ya uboreshaji wa radha ya keki.
Alisema
maonesho mengine yatakayofanywa na wadau hao wa keki ni pamoja na
uhifadhi bora wa keki kwa muda mrefu bila kuharibika na washiriki
kuonesha maumbo mbalimbali ya keki yenye mvuto kwa watumiaji wa keki na
jamii nzima.
Alisema maonesho hayo yanayodhaminiwa na Azam watengenezaji wa unga bora
kwa ajili ya kutengenezea bidhaa hiyo, yatawashindanisha wadau wa
uandaaji keki na pia washindi watakao tajwa na majaji wa maonesho
watajipatia fedha
taslimu na bidhaa mbalimbali.
"...Onesho
hili litahusisha jamii yote inayojishughulisha na utengenezaji wa keki,
upambaji wa keki, wauzaji wa keki na wanaojishughulisha na bidhaa
mbalimbali zinazotumika kutengeneza keki kama vile unga wa ngano wa
Azam,"
alisema Mkurugenzi wa Insights Productions Limited, Bi. Elias.
Akifafanua
zaidi Mkurugenzi huyo alisema onesho hilo litajumuisha bekari na hoteli
mbalimbali, Vyuo vya taaluma ya hotelia toka Tanzania na majirani
(Afrika Mashariki) pamoja na watengenezaji keki binafsi. Wananchi
watakaotembelea maonesho hayo ambayo hayata kuwa na kiingilio watapata
fursa ya kujionea aina na mitindo mbalimbali ya utengenezaji wa keki
pamoja na kuonja bidhaa hiyo kwenye maonesho ambayo yatafanyika Serena
Hoteli jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia
maonesho hayo Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya
SSB, Mohammed Ramadhan alisema Azam ikiwa ni kampuni inayotengeneza unga
bora wa kutengenezea keki imeamua kudhamini ikiwa ni ishara ya kutambua
taaluma hiyo ya uokaji keki nje na ndani ya Tanzania.
TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA GIZ
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Michael John akitoa
tamko kuhusu Siku ya Soko la Afya iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa
kushirikiana na Shirika la GIZ , itakayofanyika Oktoba 2 katika ukumbi
wa Diammond Jubelee jijini Dar es salaam.
Naibu
Meneja wa Miradi ya Afya wa GIZ Bw. Christian Ptleiderer akizungumza na
waandishi wa habari kutoa wito kwa mashirika mengine yanayotoa huduma za
afya nchini kuendelea kusaidia na kusambaza huduma zao katika maeneo
yenye changamoto ya miundombinu na uhaba wa watumishi wa afya.Kulia ni
Mtaalam na Mawasiliano wa shirika la GIZ nchini Bi. Vida Mwasalla. Picha
na Aron Msigwa – MAELEZO.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Shirika la Ujerumani la GIZ katika uanzishaji na uendelezaji wa programu mbalimbali za utoaji wa huduma za afya zinazolenga kupunguza vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka 5.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Michael John ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akitoa tamko kuhusu Siku ya Soko la Afya nchini iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Ujerumani la GIZ itakayofanyika Oktoba 2, jijini Dar es salaam.
Amesema Tanzania na GIZ zimekuwa zikishirikiana katika uboreshaji wa miradi mbalimbali ya afya kwa kusogeza huduma za afya karibu na wananchi kuanzia ngazi ya taifa, mikoa na Halimashauri za wilaya.
Ameeleza kuwa mikoa ya Lindi, Mbeya, Mtwara na Tanga imeendelea kunufaika na miradi mbalimbali ya ushirikiano chini ya shirika hilo inayolenga kuimarisha miundombinu ya kutolea huduma za afya katika maeneo hayo, uimarishaji wa mifuko ya Afya ya Jamii na ushiriki wa moja kwa moja kusaidia upatikanaji na uendelezaji wa wataalam wa kutoa huduma za afya maeneo ya vijijini.
Ameongeza kuwa GIZ imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika kuhakikisha kuwa jamii inamudu huduma bora za afya kupitia Mifuko ya Hifadhi ya Afya ya Jamii iliyopo katika maeneo yao.
Aidha, amebainisha kuwa maonyesho ya siku ya Soko la Afya yatakayowahusisha wadau mbalimbali na mashirika yanayotoa huduma za afya nchini yanalenga kuwakutanisha wadau hao ili waweze kujadili changamoto za utoaji wa huduma za afya nchni, kujifunza mafanikio yaliyopatikana katika baadhi ya maeneo na kuweka mikakati ya kuyafikia maeneo mengi zaidi.
Kwa upande wake Mtaalam na Mawasiliano wa shirika la GIZ nchini Bi. Vida Mwasalla ameeleza kuwa maonesho ya mwaka huu yazilenga Wizara, Taasisi , Washirika wa Maendeleo, Makampuni, Mashirika binafsi na Wakala zinazojihusisha na utoaji na uendelezaji wa sekta ya afya nchini.
Amesema katika maonesho hayo GIZ kwa kushirikiana na Wizara ya Afya itaonyesha mikakati mbalimbali ya kuwaokoa watoto wadogo wenye matatizo ya afya, namna walivyofanikiwa kuwapata watumishi wa afya katika maeneo ya Lindi na Mtwara, maeneo ambayo hapo awali walikuwa hawakai katika vituo vyao.
Ameongeza kuwa mbali na Siku ya Soko la Afya kuhusisha huduma za utoaji wa elimu, vipimo, machapisho mbalimbali inalenga kuwaweka pamoja wadau hao ili waweze kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya kuchangia maendeleo ya sekta ya afya hapa nchini.
Naye Naibu Meneja wa Miradi ya Afya wa GIZ Bw. Christian Ptleiderer ametoa wito kwa mashirika mengine yanayotoa huduma za afya nchini kuendelea kusaidia na kusambaza huduma zao katika maeneo ambayo bado yanakumbwa na changamoto mbalimbali za miundombinu na uhaba wa watumishi wa afya.
Amesema wao kama GIZ kwa kuanzia wameanza na mikoa 4, na wanaendelea kujenga uwezo wa kuyafikia maeneo mengi zaidi kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani na Tanzania.

NSSF YATOA FURSA KWA WAKAZI WA MBEYA NA SONGEA
Kupitia
Semina za Fursa zinazoendelea kufanyika katika mikoa mbali mbali hapa
nchini, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) imekuwa ikitoa Elimu
ya Hifadhi ya Jamii kwa wananchi na kuwahamasisha kujiunga na mfuko huo
ili waweze kunufaika na mafao ya NSSF hususani matibabu bure kwa
mwanachama na wategemezi wake pamoja na mikopo kupitia SACCOS.
Fursa
nyingine kutoka NSSF ambazo mwanachama anaweza kunufaika nazo ni pamoja
na Pensheni ya uzeeni, Pensheni ya Ulemavu, Pensheni ya Urithi, msaada
wa Mazishi, Mafao ya Uzazi, mafao ya Kuumia Kazini.
Semina
hizi zinatoa fursa kwa wajasiriamali, wakulima pamoja na watu
mbalimbali waliojiajiri wenyewe na kuuliza maswali mbalimbali kuhusu
huduma zinazotolewa na NSSF na wengi hujiuga na NSSF baada ya kuona
faida zake.
"Katika
semina za Fursa NSSF inafanya uandikishaji wa wanachama wapya na pia
inatoa nafasi kwa wananchi kuuliza na kufahamu mambo mbali mbali
yanayohusu mfuko huo" alisema Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulemba.
Mpaka sasa NSSF imeshiriki katika Semina ya Fursa katika mikoa ya Geita, Ruvuma, Mbeya na Morogoro.
Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulemba akitoa mada katika semina ya Fursa kuhusu Elimu
ya Hifadhi ya Jamii kwa wananchi na kuwahamasisha wajiunge na mfuko huo
ili waweze kunufaika na mafao yanayotolewa na NSSF hususani Matibabu
Bure kwa mwanachama na wategemezi wake pamoja na mikopo kwa wanachama
kupitia Saccos. Semina hiyo ilifanyika mkoani Mbeya hivi karibuni.
Mama Dora Msechu Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchi za kinordic na Baltic alipokelewa kwa shangwe.
Muziki hadi lyamba
Wadau wakiserebuka
DJ Richie akiwa engine room
Dj Richie na Dr Erick Kalebi wakiwajibika
Mama Dora Msechu Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchi za kinordic na Baltic alipokelewa kwa shangwe.
Palipendeza...
Mbili zatosha???
Ukumbi ukiwa nyomi
Ngoma na nyimbo za kwetu
Nyomi
Ukumbi umenona