Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias
(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya
maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB,
Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias
(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya
maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB,
Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo.
Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed
Ramadhan (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited,
Marion Elias.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias
(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya
maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam.
Katikati ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB,
Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo na kulia ni Meneja Bidhaa za
Azam, Abubakar Suleiman.
KAMPUNI
ya Insights Productions Limited kwa udhamini wa Kampuni ya Azam
Tanzania imeandaa maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika
jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa uandaaji na
utayarishaji wa keki.
Maonesho
hayo yatajulikana kama 'Azam World of Cakes Exhibition'.
Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa
Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias alisema maonesho
hayo yanatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali binafsi, makampuni na
taasisi waandaaji wa keki nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya
kubadilishana uzoefu na kujifunza ubunifu zaidi wa shughuli hizo.
Bi.
Elias alisema dhumuni la maonesho hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika
Desemba 6, 2014 jijini Dar es Salaam ni pamoja na kusherehekea taaluma
ya uokaji keki kwa kuonesha ubunifu na utaalam wa utengenezaji na
upambaji wa keki bidhaa inayopendwa na watu wengi na kutumika katika
shughuli anuai za kijamii.
Alisema
washiriki wa tamasha hilo mbali na kushindanisha na kuonesha bidhaa zao
za keki pia wanatarajia kupata semina ya mafunzo juu ya utengenezaji
bora wa keki ikiwa na lengo la kuboresha zaidi taaluma zao.
Alisema washiriki hao pia watafanya maonesho ya utayarishaji wa vyombo
vya kutengenezea keki, utayarishaji wa unga wa ngano kwa ajili ya
kupikia keki, kutambua unga bora wa keki, uchanganyaji wa unga na viungo
vingine kwa ajili ya uboreshaji wa radha ya keki.
Alisema
maonesho mengine yatakayofanywa na wadau hao wa keki ni pamoja na
uhifadhi bora wa keki kwa muda mrefu bila kuharibika na washiriki
kuonesha maumbo mbalimbali ya keki yenye mvuto kwa watumiaji wa keki na
jamii nzima.
Alisema maonesho hayo yanayodhaminiwa na Azam watengenezaji wa unga bora
kwa ajili ya kutengenezea bidhaa hiyo, yatawashindanisha wadau wa
uandaaji keki na pia washindi watakao tajwa na majaji wa maonesho
watajipatia fedha
taslimu na bidhaa mbalimbali.
"...Onesho
hili litahusisha jamii yote inayojishughulisha na utengenezaji wa keki,
upambaji wa keki, wauzaji wa keki na wanaojishughulisha na bidhaa
mbalimbali zinazotumika kutengeneza keki kama vile unga wa ngano wa
Azam,"
alisema Mkurugenzi wa Insights Productions Limited, Bi. Elias.
Akifafanua
zaidi Mkurugenzi huyo alisema onesho hilo litajumuisha bekari na hoteli
mbalimbali, Vyuo vya taaluma ya hotelia toka Tanzania na majirani
(Afrika Mashariki) pamoja na watengenezaji keki binafsi. Wananchi
watakaotembelea maonesho hayo ambayo hayata kuwa na kiingilio watapata
fursa ya kujionea aina na mitindo mbalimbali ya utengenezaji wa keki
pamoja na kuonja bidhaa hiyo kwenye maonesho ambayo yatafanyika Serena
Hoteli jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia
maonesho hayo Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya
SSB, Mohammed Ramadhan alisema Azam ikiwa ni kampuni inayotengeneza unga
bora wa kutengenezea keki imeamua kudhamini ikiwa ni ishara ya kutambua
taaluma hiyo ya uokaji keki nje na ndani ya Tanzania.