Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe.William
Lukuvi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Mazishi ya
aliyekuwa waziri wa Fedha Marehemu Dk. William Mgimwa akiongea na
waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu mwili wa marehemu
kuwasili tarehe nne saa saba mchana uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Nyerere na Shirika la Ndege la Afrika ya Kusini na kuzikwa
tarehe sita katika kijiji cha Magunga mkoani Iringa. Kulia ni Naibu
waziri wa Fedha Saada Salum Mkuya.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe.William
Lukuvi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Mazishi ya
aliyekuwa waziri wa Fedha Marehemu Dk. William Mgimwa akiwaonyesha
waandishi wa habari (hawapo pichani) ratiba ya mazishi ya Marehemu
Mgimwa aliyefariki jana nchini Afrika ya Kusini alikokuwa anapata
matibabu. Kulia ni Naibu waziri wa Fedha Saada Salum Mkuya.
Katibu
Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Dk. Florens Turuka (kulia) na Katibu Mkuu
wizara ya Afya na Stawi wa Jamii Charles Pallangyo (kushoto)
wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na
Bunge Mhe.William Lukuvi (hayupo pichani) wakati akiongea na waandishi
wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu ratiba ya mazishi ya
aliyekuwa waziri wa Fedha Marehemu Dk. William Mgimwa.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe.William
Lukuvi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Mazishi ya
aliyekuwa waziri wa Fedha Marehemu Dk. William Mgimwa akiongea na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu ratiba ya mazishi
ya Marehemu Mgimwa ambapo mwili wa marehemu utawasili tarehe nne saa
saba, ibada na heshima za mwisho zitatolewa tarehe tano katika ukumbi wa
Karimjee na mazishi yatafanyika tarehe sita katika kijiji cha Magunga
mkoani Iringa.
Wapigapicha
kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakimpiga picha Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe.William Lukuvi (hayupo
pichani) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Mazishi ya
aliyekuwa waziri wa Fedha Marehemu Dk. William Mgimwa wakati akiongea
nao leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano uliopo Ofisi ya
Waziri Mkuu kuhusu ratiba ya mazishi.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo.
Na Kiza Sungura- MAELEZO Dar es Salaam
KAMATI
ya Taifa inayohusika na mazishi ya aliyekuwa waziri wa Fedha Dk.
William Mgimwa imetoa ratiba ya mazishi ambapo mwili wa marehemu
utawasili siku ya jumamosi tarehe nne saa saba mchana katika uwanja wa
Mwalimu Nyerere Terminal II na kupelekwa nyumbani kwake Mikocheni B
jijini Dar es salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera
Uratibu na Bunge) Dk. William Lukuvi alisema kamati itakayohusika na
mapokezi ya mwili wa marehemu ni ofisi ya Waziri Mkuu itakayohusika na
ndugu, viongozi na wananchi na Kamati ndogo ya mkoa wa Iringa
inayoongozwa na mkuu wa mkoa huyo Dk. Christine Ishengoma.
Dk.
Lukuvi alisema siku hiyo ya jumamosi saa kumi na moja jioni mwili
marehemu utapelekwa katika hospitali ya Lugalo na tarehe tano siku ya
jumapili saa tano na nusu asubuhi mwili wa marehemu utapelekwa katika
ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya ibada na kutoa heshima za mwisho.
Alisema
ifikapo saa nane mchana mwili wa marehemu Dk. Mgimwa utapelekwa uwanja
wa ndege wa Mwalimu Nyerere Terminal I kwa ajili ya kuelekea Mkoa wa
Iringa.
Ifikapo
saa kumi kamili alasiri mwili wa marehemu utakuwa umewasili Mkoa wa
Iringa katika uwanja wa ndege Nduli na kuagwa na viongozi na wananchi
wa mkoa huo katika ukumbi wa Siasa kilimo na baada ya hapo utapelekwa
kijijini kwake Magunga.
Waziri
Lukkuvi alimalizia kwa kusema kuwa shughuli za mazishi ya Marehemu Dk.
Mgimwa zitafanyika 6.1.2014 kuanzia majira ya saa sita mchana katika
kijiji cha Magunga mkoani Iringa na atazikwa kwa heshima zote za
Kiserikali.