Wanajeshi wa S.Kusini wakomboa Bentiu




Hli ya wakazi wa Sudan Kusini ni ya kusikitisha baada ya maelfu kukimbia vita
Taarifa kutoka Sudan Kusini zasema kuwa wanajeshi wa taifa hilo wamechukua udhibiti wa mji wa Bentiu kutoka kwa waasi watiifu kwa aliyekuwa makamu wa Rais wa nchi hiyo Riek Machar.
Msemaji wa kijeshi huko Juba ameiambia BBC kuwa majeshi ya serikali kwa sasa yamechukua usukani wa mji huo.

Hakuna taarifa iliyotolewa kuhusiana na majeruhi.Amesema kulikuwa na makabiliano madogo kwani waasi walikuwa wakitumia vifaru katika daraja moja nje kidogo ya mji huo.
Maelfu ya raia wamekimbia mji wa Bentiu ambao ni makao makuu ya jimbo lenye utajiri wa mafuta la Unity kabla ya serikali kuukomboa.
Mpatanishi mkuu katika mkutano wa mazungumzo ya kuleta amani huko Ethiopia anasema kuwa ana imani muafaka wa kukomesha vita utaafikiwa karibuni.
Na BBCSwahili