Wadau wa huduma za afya manispaa ya Tabora, wameridhia utaratibu wa huduma za matibabu za uchangiaji zijulikanazo kama tiba kwa kadi (tika) kuanza kutumika katika manispaa hiyo.
Wadau hao waliridhia utaratibu huo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa .
Baada ya kufikiwa kwa ridhaa hiyo kutoka kwa wadau hao 260 wa makundi
mbalimbali katika jamii wakiwemo viongozi wa madhehebu ya dini, watu maarufu
kinahcofuata ni kutungwa kwa sheria.
Kikao hicho pia kilichoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wanaoratibu na kusimamia huduma za mfuko wa afya ya jamii kilipata bahati ya kuhudhuriwa na wakuu wa wilaya za Iramba na Igunga waliotoa uzoefu wao namna bora ya kuendesha huduma za mfuko huo ili kupata matokeo ya haraka.
Mkuu wa wilaya ya Iramba Yahaya Nawanda aliwaelezea wadau hao kuwa ili huduma za uchangiaji za tika zifanikiwa ni vyema halmashauri ibuni miradi ya kuwawezesha wananchi kiuchumi ili waweze kuwa na uwezo wa kuchangia tika mara utaratibu huo utakaporidhiwa na kuanza kutekelezwa.
Amesema mafanikio ambayo Iramba imepata yametokana na wananchi kuziona fursa za kiuchumi na kuzitumia na kuongeza kuwa watendaji ni muhimu wakapewa posho zao na stahili nyinginezo ili waweze kutimiza majukumu yao. Aidha amesema mambo yote hayo yanaweza kufanyika kupitia mapato
ndani ya halmashauri.
Naye Elibariki Kingu, mkuu wa wilaya ya Igunga aliwataka wakazi wa manispaa hiyo kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana kwani mafanikio ambayo Igunga imepata kwa sasa yanayokana na ushirikiano mkubwa kati ya wanasiasa na watendaji wa ngazi zote.

Ilielezwa pia katika kikao hicho kuwa kabla ya kuanza rasmi
kwa utaratibu huo, vikao mbalimbali vya kuridhia maamuzi hayo ya wadau vitafanyika
ili kuufanya utaratibu huo uwe wa kusheria.
Mratibu wa huduma za Tika kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Rehani Athumani amesema tayari kamati za huduma za jamii na ile ya fedha na mipango zimekwisha ridhia rasimu ya sheria ndogo ya Tika.
Rehani amesema kinachosubiriwa kwa sasa ni baraza la madiwani kuupitisha rasmi utaratibu ambapo wadau mbalimbali wa manispaa watashirikishwa kutoa maoni kwa mara ya pili kabla ya sheria ndogo hiyo kuwasilishwa ngazi za kisheria na utawala kwa ajili ya hatua zaidi.
Manispaa ya Tabora inaungana na manispaa za Ilala, Kinondoni, Temeke na Morogoro kupitisha sheria ndogo kwa ajili ya huduma za matibabu ya tika.

Halmashauri nyingine za miji zilizopitisha utaratibu huu
katika
siku za karibuni ni Mji Kibaha, Babati, Njombe na Makambako.
Hadi tarehe 30 septemba, 2013 jumla ya halmashauri 120 kati ya 165 zilikuwa zinatekeleza huduma za mfuko wa jamii ikiwa ni asilimia 73 ya lengo la kuhakikisha halmashauri zote nchini ikiwemo mpya zilizoanzishwa hivi karibuni zinakuwa na mfuko wa afya ya jamii kabla ya mwaka 2015.
Kwa mujibu wa Rehani, halmashauri za Kaliua, Ujiji, nyasa na
halmashauri za mkoa wa katavi zitapata mafunzo kwa ajili ya kuanzisha mfuko huo Februari mwaka huu na kwamba maandalizi muhimu yanafanywa kwa pamoja katika mamlaka ya halmashauri husika na ofisi za NHIF za mikoa.