Wakuu, Leo “Jaji Warioba” ambaye ni
Mwenyekiti wa TUME YA KATIBA MPYA amehojiana na Mwandishi wa Habari wa
Kituo Cha Channel ten aliyetaka Kujua ni Kwa nini hasa Baadhi ya
Wanasiasa na Wanachama wa Vyama vya Siasa hasa wale wa Chama tawala
Wanapendekeza Serikali Mbili, huku Wakitoa Ufafanuzi Kuwa Uwepo wa hizo
Serikali tatu Utakuza Migogoro ya Muungano na hata Kupelekea Muungano
Kuvunjika!?.
Akijibu hoja hiyo ya Mwandishi Jaji Warioba amesema “Kwanza
nakuhakikishia Kwamba hoja hiyo haina Mashiko wala Umuhimu Wowote wa
Kuzuia Uwepo wa Serikali tatu, Mimi nadhani hizo ni Hoja za Kujitungia
Kama zile ya Kusema Kwamba Serikali tatu ni Gharama, Kitu ambacho
nilikwishakitolea Ufafanuzi wa Kina. Kuhusu Jambo hili, Kwani Wewe Kwa
Mtazamo wako
“Kati ya Majaji na Wanasiasa ni akina nani Wanaoijua
Migogoro ya Muungano huu!?…naomba Utambue Kwamba Majaji Wanaijua Vyema
Migogoro hii na Vyanzo vyake Kuliko hao Wanasiasa, na ndio Sababu
tunasema Suluhisho lake ni Serikali tatu ambazo haziepukiki hata
Ufanyeje. Nawasilisha!
Na Jamii Forums
Habari Online na Elimtaa
bongo news
Jaji Warioba:”Nani anayeijua zaidi Migogoro ya Muungano huu Kati ya Majaji na Wanasiasa”?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)