Sudan na Sudan Kusini zimejadili
swala la kushirikiana katika kushika doria ili kulinda visima vya
mafuta Sudan Kusini ambako waasi wanatishia usalama.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini.Taarifa hii inakuja baada ya Rais wa Sudan Omar Bashir kwenda mjini Juba kwa mashauriano na Rais Salva Kiir kuhusu mzozo wa kisiasa unaotokota nchini humo.
Mgogoro huo kati ya wafuasi wa Rais Kiir na hasimu wake Riek Machar aliyekuwa makamu wa rais wa bwana Kiir ingawa alifutwa kazi pamoja na mawaziri wengine wa serikali.
Takriban watu 1,000 wameuawa kwenye mgogoro huo uliozuka tarehe 15 mwezi Disemba.
Na BBCSwahili