Nguku anaelezea kwamba kitabu hicho yenye kauli mbiu “Sio Serikali ni Mimi, Wewe na Sisi,”inatoa hamasa kwa watu hasa hasa kundi la vijana waweze kuwa na uthubutu wa kutimiza malengo yao katika maisha. Wanaoshuhudia ni mama yake mkubwa Bi. Anna Kikwa na baba yake mdogo Bw. Emmanuel Mallewo.
Bi. Kikwa (kushoto) na Bw. Mallewo wakionyesha kitabu cha 'Safari Ya Ndoto' alichokiandika mwanao Aman (katikati) anayesoma shahada ya uchumi mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Ardhi.
Mtunzi wa kitabu cha 'Safari Ya Ndoto' Aman Nguku akihojiwa na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kitabu hicho jana. Wanaoshuhudia ni walezi wake Bi. Kikwa na Bw. Mallewo.
===== ======= ======
Vijana
wakitanzania wameaswa kuacha kulalamika na kuishi katika maisha ya
nadharia, badala yake wameshauriwa kubadilika kuwa watendaji na wenye
uthubutu wa kutimiza malengo yao katika maisha. Maneno hayo yalisemwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Amajat Investment Bw. Aman Nguku jijini Dar es
Salaam jana katika uzinduzi wa kitabu chake kiitwacho ‘Safari Ya Ndoto’
inayobeba kauli mbiu “Sio Serikali ni Mimi, Wewe na Sisi.”
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Bw. Nguku alisema imefika
wakati sasa watanzania hasahasa kundi la vijana waamke kutoka usingizini
na kutimiza malengo yao ya kimaisha ambayo wanapenda kufikia.
“Imetosha
kusema kesho, kufikiri bila kutenda na kuongea bila vitendo.
Kinachotakiwa ni kuanza utekelezaji,” alinukuu Bw. Nguku kutoka kwenye
kitabu chake chenye kurasa 108. Akielezea madhumuni ya kuandika kitabu
hicho, Bw. Nguku ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu anayesomea
shahada ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam
alisema:
“Hiki
kitabu ni mahususi kwa wale watu ambao wana ndoto mbali mbali katika
maisha yao lakini hawajui pakuanzia, iwe ndoto ya kuwa mfanyabiashara
maarufu, mwanasiasa au daktari bingwa. Hiki kitabu ni ramani maalum
kwao.”
Aliendelea,
“Kitabu hiki kinaweza pia kuwa changamoto kwa wale ambao wamekata tamaa
katika maisha. Kwa kusoma maandishi ya kitabu hiki, wanaweza wakafufua
ndoto zao na kufanikiwa katika yale waliyoyapanga.”
‘Safari
Ya Ndoto’ pia inabeba dondoo kutoka kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Nyerere, mfanyabiashara maarufu Bw. Reginald Mengi na Mkurugenzi
Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Bw. Patrick Ngowi.
Kitabu
hiki kinasambazwa katika maduka mbali mbali jijini Dar es Salaam na
nchi nzima ili watanzania wengi wapate kukisoma. Kinauzwa kwa Tsh 5000
tu. Kwa sasa, mtunzi Nguku pia anaandika vitabu vingine viwili venye
vichwa ‘Ndogo lakini muhimu, kesho’ na ‘What is life for!’ (Maisha ni ya
nini!).
Na Jiachie