Mapigano mapya yahofiwa Sudan Kusini.



Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akisalimiana na wananchi.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akisalimiana na wananchi.

Maelfu ya watu wamekimbia mji mkuu wa Sudan Kusini wakihofia mapigano mapya baina ya wanajeshi waasi na serikali.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa zaidi ya watu elfu moja wameuwawa na wengine laki mbili wamekoseshwa makazi kutokana na mapigano hayo yaliyodumu kwa wiki tatu sasa. Rais wa shirika la kimataifa la msalaba Mwekundu , Peter Maurer amemaliza ziara ya siku tatu nchini humo akitembelea makambi ya wakimbizi.

Anasema kitu kilichomshangaza ni kwamba watu walioondoka katika makazi  yao wameacha kila kitu nyuma na kwenda katika makazi mapya bila mali zao wakati huo huo mazungumzo ya amani katika nchi jirani ya Ethiopia bado hayajafanikiwa huku serikali ikikataa madai ya waasi kuwaachilia wafungwa 11 wa kisiasa.

Na Voa swahili