Amethibitisha kupatikana kwa mizigo iliyokuwemo kwenye meli hiyo na kusema mamlaka inaendelea kufanya uchunguzi wa kina juu ya idadi ya abiria waliosajiliwa ili kuona kama inaendana na abiria waliokuwemo katika chombo hicho.
Boti hiyo iliyopigwa na dhoruba kali ilikuwa na abiria 396 ambapo 60 kati yao ni watoto na kutokana na ajali hiyo watu watano wamepatikana wakiwa wamekufa huku majeruhi wakiwa ni watatu ambao walipelekwa hospitali.