HOLILI: WANARIADHA wanne kutoka Holili Youth Athletics Club
wanatarajiwa kushiriki Serengeti Marathon siku ya Jumatano Desemba 4 mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Klabu hiyo imesema wachezaji hao wanne wapo katika kambi yao
iliyoko Tarakea Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro.
Imewataja nyota hao kuwa ni
Neema Mathias na Furaha Sambeke kwa mbio za wanawake huku Baraka William na
Godfrey Charles kwa mbio za wanaume.
Taarifa ya klabu hiyo imeongeza
kuwa wanariadha wake wataungana siku ya Jumatatu Desemba 2 mwaka huu na Wakenya
kutoka Klabu ya Riadha iliyopo Machakos wenye ushirikiano mkubwa na klabu hiyo katika
mbio za Serengeti Marathon
Mpaka sasa Holili Youth
Athletics Club ina jumla ya wanariadha 14 walioko kambini kujiandaa na michuano
mbalimbali ya riadha kote ulimwengu.
Na Jaizmelaleo