WANANCHI wa kata ya Madibira wilayani Mbarali mkoani Mbeya
wameiomba Serikali kuwapelekea umeme ambao utasaidia kupandisha bei ya Mpunga
ambao unazalishwa kwa wingi maeneo hayo na kuuzwa kwa bei nafuu.
Wakizungunza kwa nyakati tofauti na Elimtaa wananchi hao walisema,
kuwa wamekuwa wakiuza kwa bei ya chini zao hilo ambalo wanauza likiwa ghafi
kutokana na kutokuwepo kwa umeme wa kuendesha mashine ya kukobolea Mpunga.
Walisema kuwa uwapo wa umeme utasaidia kuendesha mashine
kubwa ya kukoboa mpunga na kuwafanya wakulima kuuza mchele ambapo watauza kwa
bei nzuri tofauti na wanavyouza mpunga hivi sasa.
Mmoja wa wakulima hao Zachalia Mhiche alisema kuwa katika
maeneo yao kuna wazalishaji wakubwa wa mpunga na wanazalisha zao hilo kwa wingi
na kuambulia kuuza bei isiyo na tija.
Alisema, katika maeneo hayo kuna mradi mkubwa wa mashamba ya
mpunga ambayo wamekuwa wakiyalima na kupata mavuno mazuri na kukwama
kufanyamaendeleo kutokana na bei wanayouza zao hilo likiwa ghafi.
Mhiche alisema kuwa kufuatia kutokuwapo kwa umeme mashine ya
kisasa ambayo imefunga katika kata hiyo inashindwa kuendeshwa kwa umeme
unaozalishw ana Jenereta na kuifanya mashine hiyo kuwapo bila kufanya kazi.
Kwa upande wa mkulima mwingine wa mpunga ambaye ameashilika
na kutokuwapo kwa umeme katika maeneo hayo, Hasani Mwalongo alisema, kuwa
wamekuwa wakilazimika kuingia gharama kusafili na mpunga mpaka Mafinga mkoani
Njombe kwaajili ya kukoboa mpunga huo ili kuuza kwa bei nzuri.
“Tumekuwa tukifunga safari kutoka hapa madibila wilaya ya
Mbarali na kuelekea maeneo ya Mafinga ambako kunamashine kwaajili ya kukoboa na
kuuza mchele kwa bei inayo endana na ghalkama za uzalishaji wa zao hilo,”
alisema Mwalongo.
Alisema kuwa kufuatia kutoa kuwapo kwa umeme tumekuwa
tukilima kwa faida ya wafanyabiashara wa zao hilo kwani wamekuwa wakinunua kwa
bei nafuu ya shilingi 10,000 kwa debe moja la mpunga na kuuza mchele kwa
shilingi 28,000 baada ya kukoboa dembe mbili za mpunga.
Alisema, serikali ni bora ika leta umeme kabla ya kutuletea
barabara ya rami kwani umeme utawakomboa katika mambo mengi ya kimaendeleo
ukilinganisha na barabara ambayo hata sasa inapitika.